Na Sam Ruhuza
Kwa watu wanaojitambua, tumeelewa!!
Nimefuatilia mijadala mingi mitandaoni, wengi wanaongelea ubinafsi kuliko facts!
Kwenye Dini Nyumba za Ibada, wauaji, majambazi,… husimama na kuelezea uovu wao na kisha kutubu na kuacha kabisa, na jamii husamehe japo wanabaki na kumbukumbu!
Mauaji ya Kimbali Rwanda hata South Africa ubaguzi wa rangi, walitengeneza meza ya kueleza na kuomba radhi na maisha yanaendelea!
Kwenye siasa, hakuna Rafiki wala Adui wa kudumu!
Wakati wa JPM, ccm wengi tulikuwa tukiwasikia na kukubaliana na hoja zao za kukosoa mfumo na hata kushiriki kudai marekebisho ya mifumo Serikalini na Katiba mpya, lakini baada ya kuzima tu na kuingia Mama, walewale wakabadilika ghafla na kutetea mifumo na kusema Katiba sio lazima na hata sasa wanadai Tume ya Uchaguzi imefanyiwa marekebisho mengi hivyo ni poa tu!
Kumbe ilikuwa wakati ule hawakupata fursa ya kufanya mambo yao, sasa wamepata, wanabeza yaleyale waliyoyasema!
Na sasa ni zamu ya wale walionufaika na JPM na wakawekwa mbali na mfumo kulalamikia yaleyale, kwanini tusiwasikilize na wao?!
Hii Nchi hakuna mwenye hati miliki ya kuwaza na kuamua kwa niaba ya wengine, sote tuna haki ya kufikiri, kushauri na kukosoa pasipo kumbeza mwingine wala kumuona hana uhalali huo!
Polepole alikuwa kwenye mfumo na alikuwa mnufaika hadi majuzi alipoamua mwenyewe kujilipua, hakufukuzwa huyu, ametoka mwenyewe, hivyo ninaweza kushawishika zaidi kumsikia na kuelewa hoja zake kuliko yule aliyeamua kuendelea kunufaika na mfumo!
Hoja zake zina mashiko, ni vyema watu wajadili hoja kuliko kumjadili Polepole!
Ameelezea kuhusiana na wizi wa kura kutumia NIDA na kudai ndio sehemu wanayopigia na yeye analijua hilo kwakuwa na alikuwa kwenye mfumo!
Nafikiri mwezi uliopita, Tume ya Uchaguzi ilitoa takwimu za wapiga kura ambapo idadi ilionekana kubwa sana kuliko kawaida na watu walijadiliana, Kulikoni??!
Ukipitia idadi ya watu wenye umri wa miaka 18 plus na wapiga kura waliotangazwa, unaona kama kuna mfanano hivi!!
Kwenye uandikishaji kura kuna mahitaji ya namba za NIDA, ni ya nini?! Maana kwa hilo tu, taarifa zako za NIDA wamebaki nazo!
Ni kweli kabisa Polepole na wengine kwenye mfumo wa JPM walituharibia sana nchi hasa kwenye kuchafua Uchaguzi na kuibuka kila mara watu wasiojulikana vitu ambavyo hadi leo vinaendelea, wao ndio waasisi, lakini hapa tusiangalie ya hovyo aliyoshiriki, bali tuzingatia anayoyaongea!
Turejee miaka hiyo Bashiru akiwa SG ccm aliwahi kusema chama chao lazima kitumie Dola kubaki madarakani na ndio fursa yao na wanaitumia kwani bila hivyo ni rahisi kuondoka na ikitoka madarakani inaweza isirejee!
Kwenye uchaguzi mkuu mgombea mwenza wakati huo alisema, hata mkichagua upinzani, bado ccm itaunda Serikali, na ikawa hivyo!! Leo yeye ndiye mgombea wa Urais!
Majuzi hapa aliyekuwa Spika amesema kuwa hata mkiwachagua wapinzani, hawatashinda!!
Kwa tafsiri ya kawaida, maelezo ya hao viongozi kuhusu ushindi wa ccm kwenye uchaguzi kuna tofauti gani na alichoongea Polepole aliyekuwa nao??! Zaidi amethibitisha yale tuliyokuwa tunahisi kufanywa!
Yawezekana kabisa JPM angekuwa bado yupo, Polepole asingeyaongea hayo, lakini ndio hayupo sasa na ameamua kuongea, mnataka tusimsikilize??!!
Anajua system ya Uchaguzi inavyofanya kazi kuinufaisha ccm, ameamua kuiweka hadharani, kwanini tumbishie wakati yeye alishiriki na ccm ilinufaika Urais, Wabunge, Madiwani, na Serikali za Mitaa/ vijiji??! Ndio sababu ameomba sana msamaha kwa aliyoshiriki.
Ameongea hoja zenye mashiko na aliyeongea ni mnufaika wa ndani, wengine hao ni matokeo ya kunufaika!
Hakuna uchaguzi huru na haki chini ya hii Tume ya Uchaguzi kwakuwa haipo huru!
Tanzania ni yetu sote! 🇹🇿🤝💪

