Kishindo cha SAFARI chaitikisa CCM NGARA, ACT WAZALENDO yatabiliwa kuibeba Kata ya Murusagamba Oktoba 29.

By Titho Philemon Sep 25, 2025

Zikiwa zimebakia Takribani Siku 34 kuelekea siku ya uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani nchini Tanzania, hali ya kisiasa ndani ya Jimbo la Ngara Mkoani Kagera yazidi kuwa Mbaya.

Wananchi wa Kata ya Murusagamba wazidi kuonyesha mahaba mazito dhidi ya Mgombea wa Udiwani kupitia Chama cha ACT WAZALENDO Ndugu SAFARI BULUNKUMA KAGIYEHE tofauti na Matarajio ya wengi kwamba angependwa zaidi Ndugu KADAGA KAFUKO KABUDIDI Mgombea udiwani kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho ni Chama tawala kwasasa.

Wananchi wa Kata ya Murusagamba wakiongea na Ngaratv.com wamekuwa na Hisia Mseto kuhusu nani anayewafaa katika uwakilishi wa Udiwani ndani ya Kata hiyo kwa Mwaka 2025/2030 huku baadhi yao wakisema wamechoshwa na taratibu za kuchaguliwa Mgombea na Chama cha Siasa tena watu wachache wenye Maslahi binafsi ndani ya chama na badala yake wanahitaji kiongozi aliyechaguo la wengi na wanayeamini atawawakilisha kwa haki bila kujali anatokea katika chama gani cha siasa.

Akiongea na Wananchi wa Kata ya Murusagamba katika Moja ya Kampeni zake NDUGU SAFARI BULUNKUMA KAGIYEHE anasema,
Nanukuu ;-
“Nilisema Nitajenga Nyumba ya Walimu, nimejenga kwa gharama zangu nyumba iko pale.. (wananchi wanamshangilia kwa makofi na Vigelegele)”.

Hoja za Mgombea huyo wa udiwani aliyekuwa Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Murusagamba kwa Tiketi ya CCM kabla hajahamia ACT WAZALENDO mapema Mwaka huu, zinaonekana kuwa na mvuto na Mashiko kwa wananchi kwa kile wanachoeleza kuwa Ndugu SAFARI BULUNKUMA amethubutu kufanya Makubwa kwa nafasi ya Uenyekiti wa Kijiji aliyokuwa ameaminiwa nayo na hivyo jamii inaamini atafanya Makubwa kwa Manufaa ya Kata hiyo pale atakapoaminiwa na kupigiwa kura za ushindi.

Aidha, kwa upande mwingine wananchi na Wana CHAMA wa CCM KATA ya Murusagamba wanaeleza kuwa baada ya Ndugu SAFARI BULUNKUMA KAGIYEHE (ACT WAZALENDO) kugombea udiwani na kuonekana kuwa na Nguvu, safari na ziara za uongo wa CCM (W) NGARA zimekuwa hazikatiki katani humwo na hivyo wanauomba uongozi wa CCM (W) NGARA kukazana kuomba kura za Rais tu kwakuwa wanaamini maamuzi ya Diwani Bora kwa Kata yao yako mikononi mwao na siyo mikononi mwa CCM wala mikononi mwa Ushawishi wa wageni ndani ya Kata hiyo.

Mmoja wa Makada wa CCM akiongea na Ngaratv.com kwa masharti ya kutotajwa majina yake anasema, namnukuu;-

“Katibu wa CCM (W) Ngara na Jopo lake walifika hapa Murusagamba kwenye ujio wa Mgombea Ubunge wa Jimbo la NGARA mapema Mwezi huu na Alitutambua wananchi wa Murusagamba kama Watu WASOMI, na TUSIODANGANYIKA, na tukainua mikono juu kama ishara ya kuunga Mkono HOJA yake hiyo, kwahiyo SISI TUNAJITAMBUA, na CCM NGARA wanalijua hilo, na kwa kipindi hiki tunaenda kuongozwa na Nguvu ya Mtu na siyo Nguvu ya CHAMA” Mwisho wa Kunukuu.

Hadi sasa bado kuna Sintofahamu ya Nani kuutwaa Udiwani Kata ya Murusagamba Mwaka huu japo Hali ya Ushawishi wa Mgombea wa Udiwani kwa Tiketi ya CCM bado iko chini na inahitaji Jitihada za Dhati kwa Chama husika kabla kipenga cha uchaguzi hakijapuulizwa.

Hiyo ndo hali HALISI ya Murusagamba kwasasa.

Endelea kutufuatilia Ngaratv.com kwa Taarifa na Habari zaidi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *