Hii ni Habari njema kwa Wananchi wa Ngara baada ya kupata Gari la Zimamoto.
Uwepo wa Gari hilo ni habari njema kwani litasaidia kuokoa maisha ya wananchi na mali zao pale yanapotokea majanga ya moto.
Ifahamike kuwa Wilaya ya Ngara ipo mpakani mwa Nchi mbili za Rwanda na Burundi ikiwa na Mipaka ya Rusumo Mugoma Kabanga na Murusagamba ambako zinafanyika Biashara mbalimbali.


