‎
‎
‎Na Juventus Juvenary – Ngara
‎
‎Mgombea Ubunge wa Jimbo la Ngara, Dotto Jasson Bahemu, ameonesha kuguswa na changamoto ya upatikanaji wa maji safi na salama katika kijiji cha Kumubuga, kata ya Nyamagoma, baada ya kushuhudia hali duni ya huduma hiyo.
‎
‎Tukio hilo lilitokea Oktoba 25, 2025, majira ya saa 10 jioni, wakati kundi la wanawake wa kijiji hicho lilipomlaki na kumweleza changamoto hiyo kwa njia ya wimbo wa kuomba msaada wa maji.
‎
‎Baada ya kusikia kilio cha wananchi, Dotto Jasson Bahemu alilazimika kuzungumzia changamoto ya maji pekee, akiahidi kuipeleka serikalini haraka iwezekanavyo.
‎
‎“Ndugu zangu wa Nyamagoma, hali hii ni mbaya sana. Haya siyo maji yanayofaa kutumiwa na wananchi wa Tanzania. Siwezi kuzungumzia masuala mengine kabla ya kuhakikisha changamoto hii inapata suluhu,” alisema Dotto Jasson Bahemu.
‎
‎Aliongeza kuwa,”Rais Dkt. Samia Suluh Hassan amekuwa akitoa Pesa nyingi sana za lutekelezairadi ya maendeleo ikiwemoiradi ya Maji hapa Nyamagoma,lakini nina uhakika haijui changamoto changamoto hii mnayokutana nay. Naomba niichukue niipeleke kwaajili ya kuotafutia ufumbuzi”.
‎
‎Wanawake wa kijiji hicho walimkabidhi chupa yenye sampuli ya maji machafu wanayotumia kila siku, na mgombea huyo akaahidi kuifikisha kwa Waziri wa Maji ili hatua zichukuliwe.
‎
‎Baada ya mkutano huo, mgombea huyo wa Ubunge alitembelea chanzo cha maji kinachotegemewa na wananchi ili kujionea hali halisi. Aliwahimiza wananchi wa Nyamagoma kujitokeza kwa wingi kupiga kura kwa wagombea wa nafasi za Diwani, Mbunge, na Rais, akisema hatua hiyo itasaidia serikali kuendelea kutatua changamoto za msingi zinazowakabili.
‎


