Mabasi kadhaa yanayodaiwa kuwa yameharibika, yameegeshwa Wilayani Ngara kwa zaidi ya miezi Sita sasa na kugeuka kero kwa wana Ngara wengi. Mabasi hayo yanasemakana ni mabasi ya Burundi.
Basi la Kwanza lipo Nakatunga, na la pili lipo K9-Ngara.
La tatu nimelipita Karagwe! Magari hayo hufanya Safari zake kati ya Bujumbura -Burundi na Kampala-Uganda.
Mabasi ya Burundi ambayo yamefia Ngara yamezua kero na hofu kuwa peingine yanatumika kuperereza Ngara na Kagera kwa ujumla. Kwenye mitandao ya kijamii kumekua na maongezi, ambayo hatuna uhakika nayo, kuwa nchi kadhaa zilizozunguka mkoa wa Kagera zimekua zikinyemelea kunyakua mkoa wa Kagera ama pengine kurekebisha mipaka ya nchi zao kwa kumega ardhi ya mkoa wa Kagera.
Yameharibika, zaidi ya Miezi 6 na hakuna jitihada za wazi zinazoonekana kuyashughulikia. Wasiwasi ni kwa Wananchi wa maeneo yalipoegeshwa Mabasi hayo…… Kulikoni?
Magari mabovu huhifadhiwa gereji ama sehemu maalumu kuegesha magari. Ila Wilayani Ngara, mabasi kadhaa ya kutoka nchi jirani yameegeshwa kando kando mwa bara bara katika vijiji mbali mbali Wilayani Ngara. Kwa usalama wa wilaya, ni vizuri haya mabasi yaondolewe pembembeni mwa bara bara na yakaegeshwe kwenye gereji na sehemu zilizowekwa kwa kuhifadhi magari. Ka magari ambayo hata sio ya wana Ngara ama Kagera kuegeshwa pembenzoni mwa bara bara yanaweza kutumika kama maficho ama vichochoro ya uvunjifu wa sheria na hata zinaa.
Baada ya kuwa njia za usafiri kwa wananchi, mabasi haya yamekua vyanzo vya kero na hofu kwa wana Ngara wengi.
Kwa viongozi wa Wilaya ya Ngara, ni kwamba tuseme gerezi na sehemu za kuegesha magari zimejaa mpaka kuruhusu magari kuegeshwa pembezoni mwa bara bara?
Taharuki kwa wananchi zitaisha haya magari yakihifadhiwa sehemu sahihi ambapo yatapewa ulinzi sitahiki.