DIWANI WA NGARA MJINI ASHIRIKI USAFI WA MAZINGIRA PAMOJA NA WANANCHI

By Na Mwandishi Jun 8, 2026


Diwani wa Kata ya Ngara Mjini, Kennedy Stafford Festo, ameungana na wananchi katika shughuli za kujitolea kufanya usafi wa mazingira kwa kushiriki kazi mbalimbali za mikono.


Katika picha, diwani huyo anaonekana akiwa katikati akishiriki kusafisha mtaro kwa kutumia jembe, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuboresha mazingira na kuimarisha usafi wa mazingira katika mji wa Ngara.


Shughuli hiyo imefanyika katika barabara ya NMB Benki kuelekea Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ngara, ambapo wananchi na viongozi wameendelea kuhamasishwa kushiriki shughuli za maendeleo na utunzaji wa mazingira.


Picha na Nuru Christopher Nzoya.