IFAHAMU HISTORIA YA MFUKO HUU MDOGO KWENYE JEANS

By Na Mwandishi Apr 13, 2026

UNAJUA NINI KUHUSU MFUKO MDOGO WA JEANS?

Watu wengi wanavaa Jeans, ila ukweli hawaujui mfuko huo mdogo ndani ya mfuko wa jeans na hawaijui historia ya yake ambayo inavutia!.

Mfuko huu Kiingereza unaitwa Watch pocket (mfuko wa saa) Au coin pocket (mfuko wa sarafu).

Historia ya mfuko huu ni ya muda mrefu. Ulianza karne ya 19 na kampuni ya Levi Strauss & Co. walipotengeneza jeans za wafanyakazi (hasa wachimba madini).

Wakati huo watu wengi walikuwa wanatumia saa za mfukoni (pocket watches), hivyo Mfuko huu uliwekwa ili kulinda saa isiharibike au kupasuka wakati wa kazi ngumu.

Matumizi yake siku hizi yamebadilika kidogo ambapo kwa sasa watu huutumia Kuhifadhi sarafu,Kuweka funguo ndogo,Kadi au vitu vidogo na wengine hata huweka USB au pete.
Kwa kifupi

Zamani ulikuwa wa kuweka saa, Sasa: ni mfuko wa vitu vidogo.