Ngara, Tanzania — Tovuti ya www.ngaratv.com inaungana na wananchi wa Wilaya ya Ngara katika kuomboleza msiba wa kijana mashuhuri na mfanyabiashara maarufu, Kalist Mboya, ambaye amekuwa nembo ya juhudi, ubunifu na maendeleo katika eneo hilo.

Kalist Mboya, anayefahamika pia kama KM ENERGY kutokana na mafanikio yake katika biashara ya mafuta kupitia vituo vyake vya Mugoma na Nakatunga, alijipatia heshima kubwa kwa mchango wake katika sekta ya biashara na usafirishaji. Mbali na vituo vya mafuta, pia aliacha alama kupitia biashara ya magari na miradi mingine ya kiuchumi ambayo imekuwa ikinufaisha jamii ya Ngara.

Kwa masikitiko makubwa, maisha ya Kalist Mboya yamekatishwa ghafla kufuatia ajali iliyotokea hivi karibuni katika eneo la Kasharazi, Wilaya ya Ngara. Uongozi wa Ngara TV unaungana na familia, ndugu, marafiki na wananchi wote katika kipindi hiki kigumu cha maombolezo.
Mungu amlaze mahali pema peponi.
Raha ya milele umpe ee Bwana, na mwanga wa milele umuangazie.

