Lifahamu Daraja la Ruvuvu: Hitoria na Chimbuko la Jina Lake.

By admin Mar 9, 2026

Wilayani Ngara mkoani Kagera Region kuna daraja muhimu linalojulikana kama Daraja la Ruvuvu, mojawapo ya miundombinu yenye historia ya kipekee katika eneo hilo.

Daraja hili lilifunguliwa rasmi tarehe 17 Agosti 1980 na Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Julius Kambarage Nyerere.

Tangu wakati huo limeendelea kuwa kiungo muhimu cha usafiri na mawasiliano kwa wananchi wa maeneo ya Ngara  na maeneo jirani.

Daraja hili linanaunganisha Kata mbili ambazo ni Kabanga na Mbuba,kupitia vijiji vya Djururigwa na Kumwendo.

Hata hivyo, licha ya kuitwa Daraja la Mto Ruvuvu katika kumbukumbu rasmi, baadhi ya wakazi wa eneo hilo wanasema jina sahihi kwa mujibu wa asili ya wenyeji ni Ruvubu.

Akizungumza na chombo hiki cha habari, mkazi wa Kijiji cha Kumwendo, Bwana Elibariki Minani, alisema kuwa jina hilo lina tafsiri ya kihistoria inayotokana na mazingira ya mto huo.

“Wanaliita Ruvuvu, lakini sisi wenyeji tunajua ni Ruvubu,” alisema Minani.
Kwa mujibu wa maelezo yake, zamani mto huo ulikuwa na viboko wengi. Katika lugha za makabila ya wenyeji wa eneo la Ngara — hususan Washubi na Wahangaza — kiboko huitwa Imvubu.

Kutokana na uwepo mkubwa wa wanyama hao, wenyeji waliuita mto huo Ruvubu, likiwa ni jina linaloashiria mahali palipokuwa na viboko wengi.

Leo hii, Daraja la Ruvuvu linaendelea kuwa sehemu muhimu ya historia na utambulisho wa eneo hilo, huku simulizi za wenyeji zikisaidia kuhifadhi kumbukumbu na chimbuko la majina ya maeneo yao.

Je, wewe unafahamu historia au simulizi nyingine kuhusu Mto Ruvuvu/Ruvubu na daraja lake?

Tuma maoni yako ili tuendelee kuandika na kuhifadhi historia za maeneo yetu. 

By admin

This website stores cookies on your computer. These cookies are used to provide a more personalized experience and to track your whereabouts around our website in compliance with the European General Data Protection Regulation. If you decide to to opt-out of any future tracking, a cookie will be setup in your browser to remember this choice for one year.

Accept or Deny