Wana Ngara Tuungane Kuijenga Ngara Yetu
Kumekuwa na mtazamo unaojirudia miongoni mwa baadhi ya wana Ngara kuwekeza na kujenga zaidi katika miji mikubwa kama Dar es Salaam, Mwanza na Arusha, huku Wilaya ya Ngara ikibaki kuwa sehemu ya kurejea wakati wa sherehe au misiba.
Ni jambo la kawaida watu kutafuta fursa za elimu, biashara na ajira katika maeneo yenye miundombinu na masoko makubwa.
Hata hivyo, hali hiyo inapoendelea bila mkakati wa kurudisha uwekezaji nyumbani, huweza kukwamisha kasi ya maendeleo ya eneo la asili.
Wapo wana Ngara wenye majumba ya kifahari, magari mazuri na miradi mikubwa ya uwekezaji katika mikoa na majiji yaliyoendelea.
Lakini swali la kujiuliza ni hili: Je, Ngara ni sehemu ya maziko ? au ni nyumbani panapostahili pia kupambwa na kuendelezwa?
Ukiachilia mbali misiba na sherehe, kuna haja ya kuhamasisha:
i. Uwekezaji wa viwanda vidogo na vya kati Ngara.
ii. Uboreshaji wa sekta ya elimu kwa kuanzisha shule bora binafsi.
iii. Uwekezaji katika kilimo cha kisasa na biashara.
iv. Kuibua miradi ya utalii na huduma za Usafiri.
Maendeleo ya Ngara hayataletwa na wageni pekee; yanahitaji nguvu, mtaji na mawazo ya wana Ngara wenyewe, popote walipo.
Kuijenga Ngara hakumaanishi kuacha kuishi au kuwekeza nje, bali ni kuhakikisha sehemu ya mafanikio inarudi nyumbani.
Niwaombe Tuungane, tuwekeze nyumbani, tujenge ajira kwa vijana wetu na tuifanye Ngara kuwa mahali pa fursa si pa kupita tu wakati wa matukio.
Ngara ni yetu. Maendeleo yake ni jukumu letu.
Wenu, Mlevi anayeipenda Ngara.

