Katika hali ya kushangaza Leo iliyo tikisa ulimwengu ni hiki alicho fanya mtoto wa raisi wa Cameroon.
Brenda Biya, binti wa Rais wa Cameroon Paul Biya, ameweka historia kwa kutoa tamko la kisiasa la kutaka Wacameroon wasimchague baba yake katika uchaguzi wa urais unaotarajiwa kufanyika Oktoba 2025.
Akiwa kwenye matangazo ya moja kwa moja kupitia TikTok, Brenda ambaye pia anajulikana kwa jina lake la kisanii “King Nasty”, alimlaumu baba yake kwa utawala wa miaka 43 uliosababisha umasikini mkubwa, ukosefu wa ajira na kudorora kwa uchumi nchini Cameroon.
Paul Biya, mwenye umri wa miaka 92, ni miongoni mwa viongozi waliodumu madarakani kwa muda mrefu zaidi duniani, kwani amekuwa rais tangu mwaka 1982. Urais wake mara nyingi umekuwa ukikosolewa kwa mienendo ya kiimla, ufisadi na matokeo ya uchaguzi yenye utata.
Je hii inawezekana Kwa nchi yako mtoto wa raisi kuongea hivyo hadharani?

