‎Na Ndaisaba Mchiro-Murusagamba
‎16/20/2025.
‎
‎Oktoba 29,2025 Watanzania watapiga kura kuchagua viongozi mbalimbali akiwemo Rais, Wabunge na Madiwani.
‎
‎Zoezi hilo litafanyika, baada ya Kura za maoni zilizofanyika 04/08/25 ambapo Madiwani na Wabunge wateule wa sasa walipigiwa kura.
‎
‎Katika jimbo la Ngara, nyota ya ushindi iling’ara kwa kijana Dotto Jasson Bahemu mwandishi wa habari na mtangazaji wa Clouds Media Group ambaye mpaka sasa ndiye mgombea Ubunge pekee aliyepita bila kupingwa.
‎
‎Ni ushindi wa Kimbunga na kihistoria baada ya Mbunge aliyemaliza muda wake kijana pia Ndaisaba Ruhoro ambaye licha ya kuomba ridhaa tena Chama kilifabya maamuzi na kufyekelea mbali jina lake katika uteuzi wa wagombea 6!.
‎
‎
‎Vyanzo makini vya taarifa vinamtaja Ruhoro kama kivuruge!! Naaam.. . Kivuruge haswaa ambaye mzimu wake mpaka sasa unakiyumbisha Chama Cha Mapinduzi.
‎
‎”Pale Murusagamba kwa Babu yangu mzee Mkubila Sudi, tazama kinachoendelea wewe mwenyewe jaribu kupima tu kwa akili ya kawaida”.. .. anasema Mzee Simon Mitumbikwa mmoja wa wazee waliozungumza na gazeti hili.
‎
‎Kata ya Murusagamba ni moja ya Kata kati ya 22 za Jimbo la Ngara. katika kinyang’anyiro cha kura za maoni, aliyepitishwa na Chama cha Mapinduzi ni Bwana Kadaga Kabudidi Kafuko!.
‎
‎Ushindi wa Kabudidi Kafuko ulipelekea hasira za wanachama na wananchi wengine kumshawishi aliyekuwa mwenyekiti wa Serikali ya kijiji cha Murusagamba Bwana Safari Barunkuma Kagiyehe kuchukua fomu kupitia chama cha Upinzani ili agombee Udiwani.
‎
‎Safari,kijana mwanasiasa na anaekubalika kwa wananchi wa rika zote akaisikiliza sauti ya wananchi, akawakubalia na nakavuta fomu kupitia chama cha ACT WAZALENDO na sasa mambp ni moto balaaa.
‎
‎Ni kufuatia hali hiyo, Bwana Ndaisaba anapohusishwa na Siasa za Murusagamba ambapo wenyeji wanasema upangaji wake wa Safu kupitia kwa mratibu wake anaejulikana kama Matius Mgatha alianza kumpanikiza na kumuandaa Kadaga kugombea udiwani.
‎
‎Mleta taarifa ambaye jina limehifadhiwa anasema, “Mgatha anautafuta udiwani 2a Kata ya Kanazi, na mwenye pesa ni Ndaisaba ndiomaana Kadaga anapewa nguvu ili uchaguzi ukiisha Kadaga ampigie kura Mgatha kuwa mwenyekiti wa Halmashauri”.
‎
‎Ramadhani Nzomukunda anasema ” mchezo ulianzia kwenye Uchaguzi wa Chama ambapo Kadaga kama ni pesa alipewa za kutosha kuhakikisha anakuwa katibu wa kata yetu,na baadae kugombea udiwani yote ya asababishwa na mbunge Ndaisaba”.
‎
‎Inasemekana, Ndaisaba alikuwa na timu yake ya madiwani aliowapambania kuhakikisha wanashinda kura za maonu,na kuna wagombea wengine aliola,imika kutumia kila aina ya mbinu kuwa piga chini.
‎
‎Wapo wanaolia machozi kwakuumizwa na Ndaisaba, we zungukia kata zote utaupata ukweli, hata huyo Safari alikuwa rafiki wa Ndaisaba ila alimgeuka fasta!!!! ….anasema Kijana mwanasiasa ambae hataki kuandikwa.
‎
‎Uchunguzi unaoendelea kufanywa na gazeti hili unabaini ukweli kuwa licha ya Bwana Safari kupitia mlango wa pili bado upepo wake ni mzuri na huenda akawa Diwani pekee kupitia Upinzani katika Baraza la madiwani lijalo 2025-2030.
‎
‎Msomaji wetu, tu akuahidi kukusogesea kila habari inayoendelea kuhusu uchaguzi wa Diwani hapa Murusagamba.
‎

