Ukapela Kwaheri – Irambona na Marietha

By admin Dec 27, 2025
Ndugu Juventus Juventus akihakikisha kama radha haijabadilishwa na urembo, na mng'ao uliopo mbele yake.

Jana tarehe 26 December 2025, ilikua ni siku kubwa sana kwa mwandishi wa Habari mmoja ambaye alikabidhiwa jiko na kuuaga ukapela. Mwandishi huyo ni Juventus Juvenary Irambona ambaye pia anasemekana kuwa ni mtu mwenye bahati sana katika mwaka 2025. Mafanikio makubwa menigne ambayo ndugu Irambona aliyohakihakikisha yamemuangukia ni pamoja na kutikishitua masikio ya wana Ngara wengi pamoja na nyuzi za media nyingi alipotangazwa kama katibu msaidizi wa Mbunge wa Ngara mheshimiwa Doto Bahemu. Vile vile, ndugu Irambona alivishwa kofia ya kuwa ofisa wa habari katika himaya ya mbunge huyo.

Ni wana Ngara wangapi wanapata cheo cha nguvu, na hapo hapo wanaoa? Si kuna wengine walikua wakinong’oneza eti jamaa kaishiwa na anashindia matapu tapu na pombe za kienyeji? Kumbe aliyekua akitunza kimya kimya na kuhakikisha ngozi inang’aa ni Bi Marietha. Yote ni maisha tuu, mengi yanayosemwa yanaonyesha uhalisia wa binadamu wanaotunzunguka ila mwaka 2025 unavyofunga, ukapela nimetupia kule na mzee nimerui kwenye game. Yasemwayo hayatoisha, ila maisha lazima yasogee kwani ni kawaida kupanda na kushuka milima na mabonde katika maisha yetu. Kuanzia majirani tuliokua tunafungiana mageti na kuchunguliana madirishani mpaka kwa washikaji tuliokutana kupokezana glasi kwenye minyeso, kwa wazazi, ndugu, na marafiki walionishika mkono hadi hii siku kwenda kama ilivyopangwa, sina cha kuwarudishia zaidi ya fadhila na maombi. Tuendelee kuwa pamoja na ya nyuma tuyasahau bali tugange yajayo. Bi Marietha ni wangu kihalali!

Zifatazo ni picha mbali mbali zinazoonyesha mbwe mbwe na miondoko ya staili kabambe katika harusi yake na Bi. Marietha Mathew. Timu nzima ya Ngara TV inawatakia ndoa njema, maisha yenye neema na mafanikio tele.

Ndugu Juventus Juventus akihakikisha kama radha haijabadilishwa na urembo, na mng’ao uliopo mbele yake.

.

Ndugu Irambona akipapasa kama kweli ni chombo kimekamilika ama kama ameletewa zaga zaga za kichina.
Uhakikiki ukiendelea huko Wilayani Ngara.
Kwa kuwa bwana amesharidhia na kupokea jiko kwa mikono miwili, basi hamna tena wa kujaribu kupindua jimbo kwani kama mikuki yoote imekwepa, acheni wawili hawa waanze maisha yao ya amani.

Baada ya kuhakikihi, basi akimuongoza bi Marietha Mathew Ukimbuni.
Wawili waliopendana na kukubariana kuacha ukapela wakiingia ukumbini.
Akisalimia waliohudhulia huku akicheka kuwa hakika hiki nicho chuma. Walionuna, tupisheni, njia ni yetu, huu ni muda wetu.

Ngoja tuusakate, oneni tulivopeneza na tulivyojumuisha ndugu na jamaa ili tutangazie ulimwengu kuwa sie hatuko tena sokono. Elekezeni macho kwingine, muache tuusakate na tuishi maisha yetu.
Yawezekana mkawa hamjui, ila oneni huyu hata kanibebea koti, hakika huyu ndie niliemchagua na nitakayezeheka naye. maisha ni kusaidiana kwani nambebea ua na yeye ananibebea vingine. Maisha yaendelee.
Siku tuliokua tumesubiria ndio hii, vyakula ni vingi, muziki tumeusakata, jamii na familia tumeziunganisha na kuziunganisha. Hii shughuli isingefanikiwa kama isingekua nyie wote mliofika hapa na hata wale ambao hawakufika hapa. Kamati zoote, jamani mlichokifanya sio kidogo na itakua ni utoto kutotambua mchango wenu.

Aisee sijui nianzie wapi, ila nawashukuru kwani kuandaaa hii shughuli yote ilikua sio kazi ndogo. Neema na maombi yenu, michango na misaada yenu imefanikisha hii shughuli na tunawashukuruni. Tuendelee kuombeana na kusaidiana. Mungu ni mwema siku zote.

By admin