MWANDISHI WA HABARI EDITHA CARLO AFARIKI

By Na Mwandishi May 6, 2026


Nimepokea kwa masikitiko na majonzi makubwa taarifa za kifo cha mwandishi wa habari mwandamizi na mkongwe, Editha Carlo. Hakika kifo ni fumbo, na sisi sote ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake tutarejea kwa wakati alioupanga Yeye.
Tunamshukuru Mungu kwa maisha yake hapa duniani, maisha ambayo yalimpa nafasi ya kuwa sauti ya wasio na sauti. Kupitia kalamu na kazi zake, ameacha alama isiyofutika, huku mchango wake ukiwa na matokeo chanya kwa jamii.
Tutamkumbuka kwa uadilifu wake, weledi na uzalendo katika taaluma ya habari.
Tangulia Editha, pumzika kwa amani