UTALII WA NDANI, VIJIJINI KWETU


Ni zaidi ya kilomita 100 kutoka Ngara Mjini kwenda Murusagamba. Safari hii inakupa fursa ya kuona mandhari nzuri ya vijijini, hewa safi na maisha halisi ya wananchi wetu.


Pichani ni Juventus Juvenary mwenye Koti rangi nyekundu na Fadhili Mpanju. Picha hii ilipigwa Mukalinzi, njiani kurejea kutoka Murusagamba. Ni moja ya maeneo yanayodhihirisha uzuri wa utalii wa ndani na hazina ya mazingira tuliyonayo katika Wilaya ya Ngara.


Hakika, wakati mwingine huhitaji kwenda mbali kutafuta vivutio; uzuri wa asili upo hapa hapa vijijini kwetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *