🇹🇿 UJUMBE WA KUMBUKIZI YA NYERERE DAY 🇹🇿

By Na Mwandishi Oct 14, 2026

BILA SHAKA MKO SALAMA, NDUGU ZANGU WANANGARA NA WATANZANIA WOTE.

Leo, Oktoba 14, 2026, naungana nanyi pamoja na Watanzania wote katika kuadhimisha kumbukizi ya miaka 27 tangu kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Katika siku hii muhimu, tunakumbuka na kuenzi mchango wake mkubwa katika kujenga misingi ya umoja, amani, mshikamano, uzalendo na upendo miongoni mwa Watanzania.

Ni wajibu wetu kuendeleza tunu hizi kwa vitendo, tukidumisha umoja wetu na kushirikiana katika kujenga Taifa lenye maendeleo na ustawi kwa wote.

Roho ya Baba wa Taifa iendelee kuishi ndani yetu. Tuilinde amani, tudumishe umoja na tuijenge Tanzania yetu kwa pamoja.

Apumzike kwa amani, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
🇹🇿 MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Mheshimiwa Dotto Jasson Bahemu
Mbunge wa Jimbo la Ngara