MWANDISHI WA NGARATV. COM ACHUKULIWA NA WASIOJULIKANA

By Na Mwandishi Nov 15, 2025
Titho Philimon, ammewakilisha Chama Cha Chadema kwa muda mrefu hapa Wilayani Ngara. Alipoona anaweza kuleta maendelea kwa wana Nyamagoma kwa kudandia gari lililokua likiperekwa kwa speed inayohatarisha jamii, Titho Philimon alijiunga na Chama Cha Mapinduzi ili ahudumie wananchi kwa kuleta mawazo mapya na endelevu katika baraza la madiwani wa Ngara. Kazi alizofanya akiwa mwana chama wa Chadema zilikua zimejenga mizizi iliyoperekea wana CCM wengi kumuona kama mkosoa Serikali na kukosoa tabia mbovu ambazo wengi wao walikua wameshazizowea na kuona ni sahihi tuu ingawa hazinufaishi jamii na haziendani na sifa za kiongozi yeyote. Moja ya kazi zake, ni kusisitiza vijana wengi wajitokeza kwa wingi katika maandamano ya kukomboa nchi yao October 29th, 2025, sisitizo ambalo halikupendeza wana CCM wenzake. Vile vile, Titho Philimon amekua akianika mambo mengi yaliyochukiza jamii yaliyokua yakifanywa na viongozi hapa Wilayani Ngara. na kuperekea bwana Philimon kuwa kipaza sauti cha wengi hususani wale waliochukiza na yaliyokua yakiendelea na kushindwa kuyakemea kutokana na hofu ya kutekwa na kuumizwa. Jana, tarehe 13, November, 2025 , akiwa shambani kwenye mapumziko (Retreat), Titho Philimon alitembelewa na vijana watatu waliojimbulisha kuwa ni polis na kumkamata. Vijana hao walikua hawana pingu wala kuvaa sare za polis ila walivamia shamba na kupora kamba na kumfunga kabla ya kuondoka naye kusikojulikana. Kabla ya kumkamata, walimuita wamuonyeshe karatasi ambalo inafikiliwa lilikua ni warranty kutoka mahakamani. Titho Philimon ni mwandishi wa Ngaratv.com na kazi zake zimekua zikigusa na kuelimisha jamii.

Habari, tumepokea taarifa ya ndugu yetu Titho Philemon Dyakiye kuchukuliwa na Watu waliojitambulisha kama Askari wa Jeshi la Polisi.

Kwa mujibu wa maelezo ya Bw. Samueli ambaye alikuwa naye wakifanya kazi za Shamba hiko Murukabwe Kabingo Kakonko mkoani Kigoma. Tukio hilo lilitokea tarehe 14/11/2025 saa 5 asubuhi shambani alipokua kwenye mapumziko ya Retreat.

Samueli, msaidizi wa shambani, amesema watu hao 3 walifika kijijini Shambani wakiwa na kijana mmoja mwenyeji wa Kabingo. Kijana wa kabingo alikua ni mwenyeji na dereva wa boda boda ambaye ni msaidizi wa bwana Philimon kwa maswala ya usafiri wa hapa na pale.

Hata hivyo, jitihada za kujua alipoperekwa bwana Titho Philimon hazijafanikiwa baada ya watu kadhaa kufika kwenye vituo vya Polisi kuulizia taarifa zake na kuelezwa kuwa hayupo.