Siku chache zilizopita, minong’ono juu ya uwepo wa shindano la umiss Wilayani Ngara ilisikika toka kwenye vijiwe kadhaa vya starehe vya Ngara Mjini. Ilisemekana shindano lilikua na dhumuni la kuiwakilisha Wilaya ya Ngara ingawa zoezi zima lilikosa heshima hata ya kuwakilisha kata ya Ngara Mjini.Â
Shindano la umiss liliandaliwa kwa siri kwani marketing ya kuweka hamasa na uamsho kwa wananchi haikufanyika. Kutoweka uamsho wa shindano katika kata mbali mbali kulisababisha wana Ngara kutoshiriki kikamilifu. Taarifa za shindano la umisi wa mwaka 2026 zilisambaa kwa mfumo wa minong’ono; wakazi wengi wa Ngara walikua hawana taarifa na uwepo wa shindano hilo. Mkereketwa mmoja wa shindano hilo aliliambia gazeti hili kuwa mara nyingi haya sio mashindano kwani washindi huwa wanakua wamepangwa na lengo wanalotangaza eti nia ya zoezi zima ni kuokoa ama kusaidia mwanamke si kweli kwani kama hutoki familia fulani ama una hela, basi binti hususani kutoka kwenye kaya masikini wanachokiweza ni kupigia wengine makofi na kukodolea macho picha mbali mbali zinazosambaa kwenye vyombo vya habari. Gazeti la Ngaratv.com liliambiwa kuwa shughuli hii haifai kuitwa shindano kwani hakuna ushindano kama hata waliopewa nafasi ya kwanza na ya pili wanatoka nje ya Wilaya ya Ngara; zoezi lilikua na nia ya kutangaza hotel fulani na kukutanisha pamoja watu kadhaa. Inakuaje shindano la Umiss siku zote lifanyike kwenye kata moja tuu na lisipewe muda wa kutangazwa katika kila kona, Wilayani? Kwani Ngara Mjini ndio sehemu pekee yenye uzuri wa kuwakilisha Wilaya ama ni hotel yenye nia ya kujitangaza tuu? Ni bora hata shindano lingefanyika chini ya migomba ili kuonyesha uhalisia wa maisha ya mwana Ngara ambapo hata wasanii wasiokua na uwezo wa kununua bia moja waweze kuonyesha juzi zao na kusindikiza dada zao kutaka safari ya kutafuta taji la Wilaya ama Mkoa kama sio taji la umiss wa Taifa kabisa, Ngaratv.com iliambiwa.
Shughuli ya kutafuta miss anayewakilisha Wilaya ni tunu kwa Wilaya nzima na vema ikabebwa na kila mwana Ngara. Kwa kuwa ni neema inayotakiwa kubebwa na Ngara wote, shindano la umiss liwe linafanyika katika kata mbali mbali na hata liwekwe kwenye viwanja vya mpira ama mashambani kama mikutano ya dini, siasa, ama hata mikutano ya kijamii inavyofanyika. Wanasiasa wangekua wanafanya mikutano yao hotelini wangeambuliwa kupigiwa kura na wapambe na chawa wao tuu, Diana alivyofikisha mawazo yake katika gazeti hili. Mashindano yanayoishona jamii ni fahari kwa Ngara na yanajenga uelewano kati ya viongozi mbali mbali wa sekta mbali mbali na wilaya za jirani. Zoezi la watu kushindana kingangari ngarai linatoa fursa za washiriki kusaka taji kwa hili na mali na kutoa mafunzo kwa washiriki watajiwa.
Kutumia jukwaa kuonyesha mabinti ambao hawaishi Wilayani Ngara wakiwa wamejificha kwenye kivuli cha uwakilishi wa Ngara ni kutothamani zoezi zima la ushindani na kuivua nguo Wilaya ya Ngara.
Mashindano kama haya hutoa fursa mbalimbali ili vivutio mbali mbali vitangazwe. Idara inayohusika na utamaduni hapa wilayani ilitakiwa ionyeshe ubora wake katika kuitangaza Wilaya ya Ngara kupitia shindano hilo. Biashara mbali mbali kama shule zingetumia fursa ya kutangaza mafunzo na malezi wanayotoa kwa mabinti ama hata malezi yanayotakiwa kulea na kumjenga kijana wa leo. Sehemu za starehe nazo zingejitangaza na kuvutia wageni na wapita njia Wilayani.
Idara inayosimamia maswala ya ulinzi ilipaswa itumie fursa kama hii inayoleta vijana pamoja kuonyesha faida za ulinzi na kusisitiza kuwa jukumu la ulinzi ni kila mtu hususani vijana. Shughuli inayoleta jamii pamoja ni zana nzuri ya kujenga uchumi wa eneo husika kama imeshirikisha watu mbali mbali.
 Swala la kuonyesha uzuri na ubora wa kiuchumi sio swala lalong’onezwa kwa watu kadhaa bali ni swala linaloleta viongozi mbali mbali ili uwakilishi halisi ufanyike na wanaojitokeza kuonyesha uwakilishi wawe ni wakazi wa eneo husika na sio kuchomekwa kwenye shindano kiujanja ujanja.
Kutokana na zoezi la kuitangaza Moorland hotel pale Ngara Mjini; Wanangara wengi wameliomba gazeti hili kuanika mambo yao ya moyoni yaliyoambatana na maswali kathaa.
Cha kwanza wana Ngara wanashukuru Moorland Hotel kwa kutoa ukumbi na kujitoa ili Ngara Mjini nayo ijumuishe vijana pamoja. Waliodhamini hili zoezi na walioandaa mkusanyiko wa zoezi zima, je walikua na nia ya kutangaza vijana na uzuri wa Ngara ama lah? Mbona zoezi zima hata wakazi wengi wa Ngara Mjini hawakua na uwepo wake? Kama nia ni kuwakilisha Wilaya ya Ngara, je hawa walioshiriki wanatoka katika kata ngapi za hapa Ngara? Je ni wakazi wa hapa Ngara kwani wengi wao wangeulizwa jina na mwenyekiti wa kijiji chao ama mkuu wa mtaa, kigugumizi na miguno ndio vingewala kwenye stage.
Ila kutokana na ushiriki wa waliokua kwenye state, ni …..
Kwamba Ngara haina mabinti wazuri mpaka kuleta mabinti toka mikoa ama wilaya jirani?
Kwamba ni pesa na hongo zinazopewa uzito kuliko uzuri wa wana Ngara katika shindano la umiss Wilayani Ngara?
Kwamba utamaduni wa Ngara unadharirishwa kwani hata washindi katika mashindano kama haya washindi wanapangwa kabla ya zoezi kuanza?
Kwamba hamna mradi unaoweza kusogea mbele bila kugubikwa na changamoto zinazobomoa baadala ta kulinda na kunufaisha dhumuni?
Kwamba ni lazima mpaka manung’uniko na malalamiko yasambae ndipo changamoto zichunguzwe?
Kwani hao wanaosemekana kupatiwa nafasi ya kwanza na ya pili kwenye mashindano ya umiss wa Ngara ni lazima wawe wametokea nje ya Ngara ndio wakubalike huko watakaposogea kushindana na washindani wengine?
Pengine jamii inayosoma hii makala ina mengi ya kuchangia ila ikaona isijisumbue na sikio lisilosikia dawa. Ila wasimamizi tuwe tunatafakari na kutimiza nia ya mradi ili jamii kwa ujumla inufaike na sio kupanga ushindi kabla hata zoezi kufanyika.
Mnarudisha jamii nyuma kwa kutoruhusu ushindani halisi ulete mshindi halali kwani hao mnaowagawia ushindi wanaishia kupondwa wanapokua kwenye mbuga za wengine.
Kwa niaba ya timu nzima ya Ngaratv.com, tunashukuru kwa kuendelea kuamini kazi zetu na sie kama daraja kati ya wananchi na viongozi, kazi yetu ni kufikisha yale ambayo yangependwa kuongelewa na pengine kutatuliwa.

