
Hapa ni Kijijini Mukarehe kwenye Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi.
Hii ni mahsusi kwa wakongwe wa Chama. Ni umri wa mtu mzima sasa.
Jiwe la Msingi katika Ofisi hiyo liliwekwa na aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kagera Ndg Pius Ngeze.
Mzee Pius Ngeze, ni mwanasiasa mkongwe kupitia Chama Cha Mapinduzi, Mwandishi wa Vitabu mbalimbali vya Kilimo, na amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Ngara.
Vibao vya namna hii ni vingi, na vingi vimechakaa vinahitaji marekebisho.
