Picha hii imechukuliwa Kijijini Buhororo, Wilaya ya Ngara. Mbuzi amefungwa mdomo ili anapotolewa malishoni asiweze kula mazao hasa mahindi na maharage.
Namna ya kumdhibiti ni kukata chupa ya maji/Plastiki na kupitisha Kamba inayotumika kumziba mdomo.


