Tunawapongeza Wanawake Wote Waliogombea Udiwani wa Viti Maalumu

By admin Jul 25, 2025
Ngugu ya Wanawake ni Neema kwa Jamii

‎

‎www.ngaratv.com kama chombo huru na tumaini la wananchi wa Ngara, kata zote 22 na tarafa zake nne, tunapenda kwa heshima na taadhima kuwapongeza wanawake wote waliothubutu kuchukua fomu na kugombea nafasi ya udiwani wa viti maalum katika Wilayani Ngara.

‎

‎Katika makala hii maalum, tunawaleta mbele ya macho ya jamii wanawake waliopambana lakini hawakufanikiwa kushinda. Hili ni jambo la kujivunia. Kupambana ni ushindi wa kwanza. Kujaribu ni hatua muhimu ya ujenzi wa jamii yenye usawa na maendeleo.

‎

‎Kwa namna ya kipekee, tunawataja wafuatao:

‎

‎Olipa Agrey Bugoke 

‎

Mwanamke akiamua, kitu kinaeleweka, Ngara Njema!!

‎Nuru Chalamila 

‎

‎Jeniva Rwezaura

‎

‎Paskazia Nyamuziga Marianus

‎

‎Editha Mwinura

‎

‎Ruth Msoni na

‎

‎Agnes Mugereza Ntaundi, 

Pamoja na wengine.

‎

‎Sisi, www.ngaratv.com tunawapongeza sana. Tunaamini kuwa nguvu, ari, na uthubutu wenu ni ishara ya mabadiliko chanya katika jamii yetu. Hamjapoteza, mmekuwa mfano wa kuigwa na chachu ya hamasa kwa wanawake wengine wengi wa Ngara na kwingineko.

‎

‎Tunaelewa wazi kuwa mmepitia changamoto nyingi – zikiwemo vikwazo vya kifamilia, kijamii, na hata kiuchumi – lakini bado mlikusanya ujasiri wa kusimama na kusema: “Naweza!”

‎

‎Tuliona pia changamoto za kiufundi, kama vile kuharibika kwa kura zaidi ya 70 katika Tarafa ya Nyamiaga. Tunawapongeza wale mliothubutu kuzungumza kwa uwazi kuhusu mchakato mzima wa uchaguzi – hususan mama LIBE, ambaye alisimama na kueleza bayana hali halisi. Huu ni ujasiri wa hali ya juu.

‎

‎Tunawahimiza wote kuendelea kushiriki katika shughuli za kijamii na kisiasa, na zaidi ya yote kujiandaa kwa uchaguzi ujao. Hii ni fursa ya kujifunza, kuimarika, na kurudi tena kwa nguvu zaidi. Ngara inahitaji watu kama ninyi – wenye uthubutu, maono, na moyo wa kujitolea.

‎

‎TUNAWATIA NGUVU NA KUWAPA HESHIMA YENU KAMILI.

‎

‎Baada ya uchaguzi ni maandalizi ya uchaguzi mwingine.

‎Msikate tamaa. Msikome kugombea. Endeleeni kusimama na kusikika.

‎

‎Kwa niaba ya wananchi wa Ngara,

‎www.ngaratv.com â€“ Tumaini la Wananchi.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *