katika sakata la kuutaka ubunge wa Jimbo la Ngara, wana Ngara safari hii wameamka na vijana wamekua wawaniaji na sio wasikilizaji wa porojo za siasa nchini kwao na hata nyubani kwao, Ngara. Kati ya 14 waliochukua fomu za kugombea Ubunge wa Ngara, zaidi ya kumi ni vijana kabisaa, yaani wana miaka chini ya 45.
Itakua sio haki kupongeza vijana ambao wanawania nafasi mbali mbali Kitaifa na hapa Wilani. Makala hii inakuletea kazi bora kabisa za wanaotumia media, na viota mbali mbali kuonyesha uwepo wao kwenye sakata la ubunge.
Zifatazo ni copy na Paste za kile kinachoendelea kusambaa kwenye mitandao mbali mbali, yaaku kutoka Ngara, born here here Ngara. The proud boys of Ngara are: Eliud Ruzige and Josias Charles the best use of the media.

Ujumbe wake kwa Wana Ngara:
WAPENDWA Ndugu wana Ngara,napenda kuwasilisha vipabele vyangu 10 endapo chama changu na wananchi wa jimbo la ngara watanipa ridhaa ya kuwa mwakilishi wao kwa nafasi ya ubunge jimbo la Ngara


Na ujumbe ufatao unatoka kwa ndugu Josias Charles
TUKIO LA AJABU KWENYE SAFARI YANGU YA KUTIA NIA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA NGARA.
Tarehe 30, June, 2025 nilichukua Form ya Kutia nia kugombea Ubunge wa Jimbo la Ngara. Kama wanachama wengine nilitii kanuni za Chama za kutoambatana na Misafara ya wafuasi japo ningesema niambatane na Misafara ninaamini ningekuwa na Msafara mkubwa na wa Kihistoria.
Siku hiyo ilikuwa siku ya Kesi ya Wananchi wa Rusumo ambao ni Viongozi wa Kamati ya Malalamiko ya Fidia ya mradi wa NELSAP….. Wananchi hawa walitamani sana kunisindikiza kuchukua Form lakini niliwasihi wasifanye hivyo maana ni uvunjifu wa Kanuni zs Chama. Niliwaomba nikitoka kuchukua Form nikaungane nao Mahakamani…. Lakini nilichelewa kuchukua Form. Wananchi hawa walipotoka Mahakamani walikataa kurudi Rusumo bila kuonana na mimi, Walinisubiri eneo la Ngara Garden ambapo walinifanyia maombi maalumu kama inavyoonekana kwenye video.
Tukio hili limeacha historia Muhimu kwa Maisha yangu maana limeonyesha upendo wa hali ya Juu wa Wananchi wenzangu kwangu.
Ahsanteni sana Ndugu zangu, Tuendelee kuombeana.
Josias Charles
Mtia nia nafasi ya Ubunge, Jimbo la Ngara.