JINSI YA KUDHIBITI MBUZI WAHARIBIFU

By Na Mwandishi Nov 5, 2025
Je, unadhibitije watoto wako wanaposhindwa kufata maagizo? Je ipi ni njia sahihi ya kumfanya mtu apokee na kufata maagizo ? Je anapokua mbishi kupitliza unamlazishaje mpaka atii?

Picha hii imechukuliwa Kijijini Buhororo, Wilaya ya Ngara. Mbuzi amefungwa mdomo ili anapotolewa malishoni asiweze kula mazao hasa mahindi na maharage.

Namna ya kumdhibiti ni kukata chupa ya maji/Plastiki na kupitisha Kamba inayotumika kumziba mdomo.