TAARIFA YA KIFO
Jina la Wellington Ntamubano si geni katika masikio ya wananchi wengi wa Wilaya ya Ngara.
Akiwa baba wa familia, rafiki wa watu wengi na mpenda maendeleo ya jamii, kifo chake kimeacha pengo kubwa lisilozibika kwa ndugu, jamaa na marafiki.
Taarifa za kifo chake zilianza kusikika majira ya jioni ya Jumapili, Machi 9, 2026, na baadaye kuthibitishwa na ndugu pamoja na marafiki wa karibu wa familia.
Jioni ya leo, kikao cha maandalizi ya mazishi kimefanyika, ambapo familia imetangaza kuwa mazishi ya marehemu Wellington Ntamubano yatafanyika rasmi Ijumaa, Machi 13, 2026.
Marehemu Ntamubano alizaliwa mwaka 1949 na amefariki dunia mwaka 2026 akiwa na umri wa miaka 77.
Taarifa zaidi kuhusu historia ya maisha yake pamoja na ratiba kamili ya mazishi zitaendelea kutolewa kupitia www.ngaratv.com�.
“Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina la Bwana lihimidiwe.”

Jina la Wellington Ntamubano si geni katika masikio ya wananchi wengi wa Wilaya ya Ngara.
Akiwa baba wa familia, rafiki wa watu wengi na mpenda maendeleo ya jamii, kifo chake kimeacha pengo kubwa lisilozibika kwa ndugu, jamaa na marafiki.
Taarifa za kifo chake zilianza kusikika majira ya jioni ya Jumapili, Machi 9, 2026, na baadaye kuthibitishwa na ndugu pamoja na marafiki wa karibu wa familia.
Jioni ya leo, kikao cha maandalizi ya mazishi kimefanyika, ambapo familia imetangaza kuwa mazishi ya marehemu Wellington Ntamubano yatafanyika rasmi Ijumaa, Machi 13, 2026.
Marehemu Ntamubano alizaliwa mwaka 1949 na amefariki dunia mwaka 2026 akiwa na umri wa miaka 77.
Taarifa zaidi kuhusu historia ya maisha yake pamoja na ratiba kamili ya mazishi zitaendelea kutolewa kupitia www.ngaratv.com