
Huyu ndiye Dark Master ambaye jina lake halisi ni Athuman Kabongo.
Mwanachemba, East Zou Empire au ABC (Another Blessed Creation) kutoka 0800 Dodoma Makao Makuu. Ni mwasisi wa Chemba Squad na East Zou.
Ana dhamira ya dhati ya kufanya mapinduzi ya kimuziki nchini Tanzania na kutengeneza ajira. Niwaombe tumpe support kwa kusikiliza project yake mpya, East Zou Republic,
inayowakilisha Jamhuri ya watu wa East Zou, Serikali ya Chemba na tawala za ABC.
Katika project hii utapata mengi sana kutoka kwa Dark Master, au ukipenda muite MC Mkomunist wa kwanza, Mwanachemba, Uncle Digital, na kwa jina la kiserikali Athuman Kabongo; mkongwe wa Hip Hop na Bongo Flava tangu miaka ya 90.
Ni kweli amekuwa kimya kwa muda mrefu bila kutoa albamu kutokana na matatizo mbalimbali, ikiwemo kuondokewa na watu wake wa karibu, jambo lililosababisha ukimya huo. Lakini sasa amerudi rasmi kwa wanafamilia wake wa kweli wa muziki wake, akiwa amewaletea albamu mpya iitwayo East Zou Republic.
Anawaomba sana vyombo vya habari na wadau mbalimbali wa muziki kumshika mkono katika ujio huu mpya wenye mwanga mbele yake, ili aweze kujikamilisha zaidi kama msanii.
Kwa kuanzia, albamu hiyo itapatikana kwa shilingi 25,000 tu kupitia Airtel Money namba 0780976949, jina Athuman Jumanne Kabongo, ili kupata maelekezo ya kupata copy yako pamoja na ID yako ya East Zou Book for Life.
Karibu sana. 🙏🙏🙏
