Chanzo Cha Kukosa Masomo ni Ukosefu wa Matibabu

By admin Feb 10, 2025
Wasamaria Wema: Athuman Hussein , 11, anaomba msaada wenu ili aendelee kupata dawa (Insulni).

FAMILIA YA BW.HUSSEIN ANTHON ANATORY MKAZI WA KITONGOJI CHA RUSEMA KIJIJI CHA MAYENZI KATA YA KIBIMBA-NGARA.

Mtoto Athuman Hussein mwenye umri wa miaka 11, aliyelazimika kuacha masomo baada ya kukosa matibabu ya ugonjwa wa Kisukari tangu mwezi wa 4 Mwaka 2024.

Historia ya Ugonjwa:- Alianza kuugua mwezi huo wa April, akalazwa Hospitali ya Nyamiaga mara 4 kwa vipindi tofauti.

Katika kipindi chote cha matiababu ya mtoto Athumani, familia imelazimika kuuza rasilimali mbalimbali kama vile Mifugo (Ng’ombe, Mbuzi) na viwanja kwaajili ya gharama za matibabu.

Maelezo mengine ya Baba mzazi, ni kwamba aliekezwa na Daktari kununua dawa ili mgonjwa aendelee kuchomwa na kutibiwa Katika Zahanati ya Kijiji iliyo karibu na nyumbani.

Aidha, kutokana na Hali ngumu ya maisha imekuwa vigumu kuendelea kununua dawa (insulin). Kwa kipindi ambacho mgonjwa amekuwa nyumbani, zimetumika shilingi 450,000/=. Kwa Sasa hawana msaada wowote.

MAOMBI

Msaada wa matibabu, wadau wamsaidie kumrudisha Hospitalini na kupewa msaada wa matibabu.

“Ukweli nawaza mengi,yaani Nina msongo wa mawazo Hadi nawaza mabaya!, jamani nisaidieni”  Baba wa mtoto.

Kwa anayeguswa anaweza kuwasiliana na Baba Mzazi wa Mtoto. Simu namba +255783928789

Jina Hussein Mandela Anthony

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *