Aliyekua Nyuma ya Ubora wa Safari Larger

By admin Feb 4, 2025
Je unamfahamu Ndugu Mathew Manyaga? Ni Kinara aliyekuwa nyuma ya ubora wa bia ya kifahari nchini Tanzania maarufu kama Safari Larger. Kushote ni ndugu Sam Ruhoza, na kulia ni ndugu Matthew Nanyaga

~ Na Sam Ruhuza

Leo 04/02 ikiwa ni kumbukumbu ya kuzinduliwa Bia maarufu Africa ya Safari Larger iliyoshinda tuzo nyingi Africa na Duniani hadi kuitwa fahari ya Africa na kujizolea sifa nyingi sana zilizoitangaza Tanzania na kuinua uchumi, lakini Je unamjua mpishi wa kwanza kuiandaa na kuitoa hiyo Bia akiwa na wazalendo wenzake?! 

Habari za jina la watu kama hawa ambao sio wanasiasa wala wasio maarufu mitandaoni kwa kizazi hiki ni nadra sana kuona Habari zao zikiandikwa na waandishi hata kuulizia historia ya kitu, mfano sehemu nyingi leo ikiwamo kampuni ya bia wametangaza sana kuhusu umri wa miaka 48 ya Safari Larger, lakini hakuna aliyegusia waliyeipika hii Bia na walipo hii leo! 

Je unamfahamu Ndugu Mathew Manyaga? Ni Kinara aliyekuwa nyuma ya ubora wa bia ya kifahari nchini Tanzania maarufu kama Safari Larger. Kushote ni ndugu Sam Ruhoza, na kulia ni ndugu Matthew Nanyaga

Huyo unayemuona pichani nimepiga nae picha juzi Jijini Moshi anapoishi Ndugu yetu Mathew Manyaga Mzalendo wa Ukweli aliyetengeneza na wenzake Bia ya Safari Larger hadi kuwa bia bora Africa na Duniani, sasa ana umri zaidi ya miaka 80 akiwa bado mwenye nguvu na afya njema kutokana na style ya maisha aliyoamua kuishi, yupo fit sana. 

Tanzania ilikuwa ikiagiza shairi la kutengenezea pombe toka nje ya nchi kitu ambacho ilikuwa ikigharimu pesa nyingi za kigeni na hivyo kupelekea uzalishaji kupungua na bia kuwa adimu hasa kipindi kile ambacho pesa za kigeni ilikuwa shida, Wazalendo wa wakati ule akiwemo Mzee Mathew Manyaga wakaja na wazo la kuzalisha zao la  shairi hapa nchini kuokoa pesa za kigeni na kukuza uzalishaji. 

Bia sahihi, bia ambayo radha yake inaonyesha ubora wa Kitanzania, bia ambayo ukiitumia haikuchoshi, bia yenye radha ya sahihi, ambayo utapiga na bado safari yako itakwenda vizuri tuu; bia hii nis Safari Larger!

Mwaka 1980, Mathew Manyaga akateuliwa kusimamia mradi wa ujenzi kiwanda cha Shairi Mkoani Kilimanjaro na yeye kupewa kazi ya kuendesha zao hilo na kiwanda. 

Mwaka 1982 kiwanda cha shairi kilianza na wananchi waliweza kuzalisha kwa wingi zao hilo na kuuza kwakuwa mteja amepatikana. 

Kiwanda hiki kiliongeza kipato sana kwa wakulima  wa Shairi na kuokoa pesa za kigeni na kukuza uzalishaji wa bia. 

Mwaka 2000 Ndugu Mathew Manyaga alistaafu ajira Tanzania Breweries Limited (TBL) na hapo TBL ilibinafsishwa na shares nyingi kumilikiwa na Kampuni ya South Africa, hivyo utawala wake ukaamua kufunga kiwanda cha shairi Moshi na kuanza kuagiza shairi toka South Africa. 

Kwa TBL kuafunga kiwanda cha shairi kilipunguza sana ajira ya Wazalendo na kupunguza kipato cha wakulima, lakini kiliongeza matumizi ya fedha za kigeni hasa Dola ya kimarekani (US$) kitu ambacho kinaumiza thamani ya TSh yetu na kuongeza uzalishaji South Africa na kuimarisha uchumi wao kwenye mauzo ya malighafi ambayo hata sisi tuna uwezo nayo kuzalisha.  

Wazalendo wa maana kabisa kama Mzee Mathew Manyaga mbali ya kwamba hawakumbukwi na jamii tena wakiwa hai, lakini pia hata mashirika waliyotumika nayo hauwasikii wakiwaongelea hata kuwapatia Tuzo za heshima ama hata shares kidogo kama appreciation kwa kazi nzuri waliyoifanya wakiwa ofisini ambayo hadi leo mchango wao upo sana! 

Happy Birthday Safari Larger

Nina hakika kabisa uwekezaji mkubwa TBL ulitokana na bia bora ya Safari Larger, basi wadau wa bia leo ukiwa unakunywa Safari Larger ya baridiiii, kumbuka sana jina la Mtaalam Brewer Mathew Manyaga ndiye anakupa hiyo burudani huku akiwa amesahaulika na wahusika! 

Watanzania lazima tuthamini wananchi wenzetu hasa wazee wetu waliojitolea kufanikisha Tanzania kuonekana kimataifa lakini leo, wamesahaulika! 

Tanzania ni yetu sote! 🇹🇿🤝💪

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *