Miradi ya Vijana Imekwamia Nyumbani kwa Mbunge

By admin Apr 2, 2025
Piki piki, bajaji na hata basikeli ni baadhi ya nyenzo ambazo zinatumiwa na serikali katika kutatua ajira kwa vijana na katika kusukuma mbele uchumi. Iwe ni kijijini ama mjini, hizi nyenzo zimerahisisha maisha na kuhimiza wananchi husasani vijana wajiari. Yanaoendelea hapa Wilayani Ngara ni tofauti na yale ambayo yanafanyika mijini. Inasemekana piki piki zilizohifadhiwa katika nyumba ya Mhe Ruhoro, Mbunge ywa Ngara, yanazuwia tiririko la mapato kwa vijana wengi na kuruhusu sifa na kiki kwa muhifadhi wa hizo nyenzo zilizoletwa kwa nia ya kukwamua uchumi wa watu wengi Wilayani Ngara.

PIKIPIKI 57 ZILIZOPASWA KUGAWIWA KWA VIKUNDI 6 VYA VIJANA NGARA KUPITIA 10%  ZIKO WAPI? NYUMBANI KWA MBUNGE?

Na: Josias Charles

Siku kadhaa zilizopita nilidokezwa na moja ya wananchi wa Wilaya ya Ngara kuhusu jambo lisilo la kawaida ambapo inadaiwa kuwa Pikipiki takribani 57 zilizotolewa kwa Vikundi 6 vya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara zimehifadhiwa Nyumbani kwa Mbunge  kwa kile kinacho onekana kama mpango mahususi wa “Drama” ya Mbunge kugawa pikipiki hizo kama sehemu ya Kujiimarisha kisiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu ujao. 

Vijana waliona wazifate piki piki zilipofichwa ili zisije kupata kutu bure huku zinaweza kuwaingizia kipato haraka haraka: Picha na mwandishi wetu kutoka Buhororo

Jambo hili lilinisikitisha sana ukizingatia kuwa Wenye Jukumu la Kutoa Mikopo ya 10% Mapato ya Halmashsuri ni Serikali Kupitia ma Afisa wa Halmashauri na sio suala la Mwanasiasa yoyote kuuteka mchakato huo. 

Lakini pia Mikopo ya asilimia 10 ya mapato ya 

ndani ya Halmashauri kwa vijana 

wanawake na watu wenye ulemavu 

inafanya kazi kama mfuko unaozunguka 

ambapo Kwa mujibu wa Sheria ya Fedha ya Serikali za 

Mitaa (Sura ya 290, Kifungu cha 37a) 

inazielekeza Halmashauri zote kutenga 

asilimia 10 ya mapato yake ya kila 

mwaka kwa ajili ya kutoa mikopo isiyo 

na riba kwa vikundi vya wanawake 

(4%), vijana (4%) na watu wenye 

ulemavu (2%). Mikopo hii inakusudiwa 

kuimarisha shughuli zinazowaingizia 

kipato wanawake, vijana na watu wenye 

ulemavu wasio na ajira rasmi na hivyo 

kuboresha maisha yao kwa ujumla.

Nyenzo za kusafiri kwa watu wengi zimerahisisha maisha na kutoa fursa kwa wengi, hususani vijana. Piki piki, maarufu kama boda boda, zinatumiwa na serikali kutengeneza ajira. Boda boda pia zinaleta changamoto kama uvunjifu wa sheria za bara barani (traffic). Pia, ajari mbali mbali ambazo zinafupisha maisha ya watu wengi na kuonyesha udhaifu wa huduma za afya zilizopo hapa Tanzania kwani ajari zinazotokana na matumizi ya boda boda zinalazimisha viongozi kufikiria na kuboresha huduma zilizopo mahospitalini.

Hivyo basi, Suala la Pikipiki 57% za Halmashauri kuhifadhiwa kinyume na utaratibu nyumbani kwa Mbunge linalenga kuzorotesha lengo mama la Kutolewa kwa mikopo hiyo kwani Pikipiki hizo zilistahili kuwa kwenye shughuli za uzalishaji mali ili kuimarisha kipato cha Vijana na pia kusaidia Vijana waliokopeshwa kurejesha mikopo kwa wakati na hatimaye kutoa fursa kwa vijana wengine kukopeshwa. 

Kwa andiko hili, ninatarajia kuona Ofisi ya Mbunge ikijitokeza hadharani na kufafanua kinagaubaga kuhusu  sababu hasa ya Kuhifadhi pikipiki hizo 57 kwenye makazi binafsi ya Mbunge na ni kwa namna gani Ofisi ya Mbunge inahusika na Mchakato wa upatikanaji na ugawaji wa Pikipiki hizo. 

Moja ya mchango mkubwa viongozi wa Halimashauri waliouleta Wilayani Ngara ila inaonekana mbunge wa Ngara anashikiria hizi fursa zisifikie vijana ili azitumie kupata kiki na azitumie kujipatia kiki ambazo ni muhimu kipindi hiki cha siasa. Hizi piki piki ni mali ya umma kwani ni zao la utendaji bora wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngara. Zisigawiwe ama kuzuiliwa kisiasa siasa kwani hizi piki piki ni za wana Ngara wote na zinatakiwa kusambazwa kwa kiusawa katika kata zote 22 zilizopo Wilayani Ngara. Hizi piki piki hazitotolewa kwa huruma na upendo wa Mhe Ruhoro kama ambavyo angependa kutaalifu umma bali zimenunuliwa kwa jasho la watanzania wote ambao ni wadau wa Wilaya ya Ngara.

Lakini pia ni matumaini yangu kuwa Ofisi zinazo husika na utoaji mikopo katika ngazi ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara zitatoka hadharani na kuelezea ni kitu gani haswa kinaendelea hivi sasa kuhusiana na Pikipiki hizo na ni sababu zipi zimepelekea pikipiki hizo 57 kuwa katika makazi ya Mbunge badala ya kuwafikia walengwa ambao ni Vikundi 6 vilivyoko katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara. 

Piki piki ambazo ilikua ziende kwa vijana zimehifadhiwa nyumbani kwa Mhe Ruhoro.

Kama mdau wa maendeleo katika Wilaya ya Ngara nina tahadharisha kuhusu athari za Kuleta siasa kwenye masuala yanayohitaji Uwajibikaji na Sheria. Ninaamini kama mchakato huu wa Utoaji mikopo ya 10% utaingiza siasa utasababisha wakopaji kutokulipa mikopo hiyo na hivyo kuathiri vijana wengine ambao walitarajia kukopa. 

Piki Piki zaidi ya 20 zikikusanya vumbi na kutu ndani ya hekaru la Mhe Ruhoro. Kwa nini ziozee hapa huku vijana wanahitaji nyenzo vitendea kazi?

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *