Dotto Bahemu akagua ujenzi wa chumba cha darasa Shule shikizi Magamba unofadhiliwa ba mfuko wa jimbo

By Na Mwandishi Aug 6, 2026

Mbunge wa Jimbo la Ngara Mhe. Dotto Jasson Bahemu, amekagua maendeleo ya ujenzi wa Chumba kimoja cha darasa pamoja matundu matatu ya vyoo katika Shule shikizi ya Magamba kata ya Murusagamba, ujenzi unaofadhiliwa na Mfuko wa Jimbo.

Mfuko wa kuchochea maendeleo ya Jimbo la Ngara chini ya Mwenyekiti wake, Mhe. Dotto Jasson Bahemu, ulitoa kiasi cha shilingi 21,000,000/= kwa ajili ya Ujenzi wa Chumba kimoja cha Darasa, Matundu matatu ya vyoo pamoja na utengenezaji wa Madawati 15, ili kuondoa changamoto ya Watoto kulazimika kutembea umbali mrefu kwenda Shule ya Msingi Murugunga.

Baada ya kukagua ujenzi huo, Mhe. Dotto ameupongeza uongozi wa Kata ya Murusagamba na Kijiji cha Magamba kusimamia vyema ujenzi huo, na kwamba ataendelea kutafuta fedha kutoka kwa Wahisani mbalimbali ili kuongeza miundombinu katika shule hiyo.