Kwa muda sasa kumejengeka tabia ya Wabongo kuogopa kuongea Ukweli na iwapo wakiongea, basi hofu hutawala kwao na wapendwa wao na kuanza kuhisi muda wowote watafikwa na taarifa ya kutisha!!
Hali hii imekuwapo na ilianza kwa wale wanaoonekana wa vyama vya upinzani lakini kidogo kidogo imepanuka hadi kwa yeyote yule na matokeo yake wote ni hofu tupu na kama unataka usalama ni aidha ukae kimya ama uwe chawa kusifia na kuabudu hata kama unaamini sio sahihi!!
Mwaka jana aliyekuwa Mwenezi ccm Taifa, Mbunge, Balozi aliandika barua kujiuzuru wadhifa wake, kisha kama Raia akaanza kuelezea mapungufu ya Uchaguzi unaokwenda kufanyika, matokeo yake kabla ya Uchaguzi mkuu, alivamiwa nyumbani kwake na kutekwa, hadi leo haijulikani yupo wapi na wala chama chake hakijawahi kuongelea hilo na familia yake ni kilio cha kutokujua kama ni mzima ama la!!
Kikaoni cha ccm, ghafla Mkiti anatoa jina la mgombea mwenza kwasababu kuwa Makamu aliyepo ameomba kupumzika!!
Bunge linavunjwa ili kwenda kwenye uchaguzi mkuu, Waziri Mkuu anatangaza nia ya kutetea ubunge wake, ghafla anajitoa!!
Uchaguzi mkuu umefanyika, kila mtu ameshuhudia kilichotokea, lakini ni Tume mpya za uchunguzi zinaendelea bila wahusika kukiri au kuwajibishwa na waliotangazwa kushinda wapo wanaendelea!!
Baada ya uchaguzi mkuu tumeshuhudia mengi mageni kama vile Spika kuonyesha nia ya kutetea nafasi yake, ghafla akaacha, Naibu Waziri Mkuu na baadhi ya Mawaziri waandamizi kutokuwapo kwenye Baraza, Waziri wa Ndani baada ya uteuzi akianza kazi nzuri kwa lugha ya kuitaka Police kufanyakazi kiueledi kwenye ukamataji, watu wakaanza kumuona anaongea lugha tofauti na Mtawala, matokeo yake, akatenguliwa na kuletwa mwenye kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa!
Baadae tumeshudia Mijadala Bungeni imekuwa dhaifu sana ni kusifia na hakuna Mijadala ya kuiwajibisha Serikali kama moja ya majukumu ya Bunge!
Kauli za Makamu Rais zinakuwa za kuvutia zaidi umma na kupata tafsiri tofauti na wenzake na kuonekana kama sio mwenzao kwakuwa wengine kauli zao zinajulikana!
Akaanza kupingwa na wenzake wa chini yake hadharani bila woga na kuanza kuitwa Yuda Bungeni, gazetini bila chama tawala wala mhusika kukemea! Hapo tukajua mambo hayapo sawa kwao!!
Jana Makamu Rais anaandika barua kujiuzuru nafasi yake ili kumpa nafasi Rais kufanya uteuzi wa Makamu mwingine kwakuwa amemuona anataka kufanya mabadiliko. Barua iliyojaa hekima kubwa. Leo chama chake kimeamua kumvua uanachama kabisa kwasababu za kimaadili ambazo hawajazielezea!!
Sisi ambao tupo nje ya hicho chama ni rahisi sana kuona mapungufu yake kuliko waliopo ndani, ni kama mpira, anayeangalia ni mchezaji mzuri zaidi!
Maswali ni mengi sana!
– Je ccm bado ni chama cha siasa?! Jibu kubwa linakuja SIO, Ni chama Dola!
– Je ccm bado inafuata misingi yake?! Jibu la haraka ni HAPANA! haina misingi bali ni kufuata na kutimiza kila kitu anachotaka Mkiti!!
– Je ccm ukiwa na mawazo tofauti na wenzako kwenye maslahi ya ujenzi wa Taifa, unaeuhusiwa??! Jibu la haraka ni HAURUHUSIWE kwakuwa anayepaswa kufikiri ni Mkiti TU!
Yaani badala ya kujenga chama chao, ndio wanakiua jumla!! Wao wakiishapà ta Mkiti ndiye Rais na ndio Uhuru wao unakomea hapo na wanataka na wananchi wote wawe hivyo kila kitu!!
Inasikitisha sana!
Bila kuongea Ukweli, basi tena, mdogo mdogo itakufikia hata wewe.
Kuongea Ukweli bila kumkwaza mtu kwa maslahi ya Taifa hata Dini inatutaka hivyo.
Tupendane, leo tukichukiana na kupotezana, kesho sote hatutakuwapo na vizazi vitaongea!
Kama Ùnasali, basi ombea sana Taifa lako na busara iwajae viongozi waondoke kuwa watawala!
Tanzania ni yetu sote!Â
Â
