Mambo 20 ya Siri – Halimashauri ya Ngara

By admin Jun 11, 2025
Siri 20 Halimashauri ya Ngara

YAFAHAMU MAMBO 20 YA SIRI YALIYOFICHIKA NDANI YA HALMASHAURI YA WILAYA YA NGARA HADI JUNE 2025 : KITASA CHA SIRI KIMEPOTEZA UFUNGUO

Dokezo la Wazi kwa Jamii ya Ngara

Na:

*Titho Dyakiye Philemon*

(Kijana Mzalendo – Ngara, Kagera)

______________________________________________

YAFUATAYO ni Mambo 20 ya Siri yaliyofichika ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara hadi Leo June 2025 *ambayo yasipopatiwa ufumbuzi wa haraka* yanaenda kuiathiri jamii ya Ngara kwa ukubwa wake na kudumaza maendeleo yake kwa ujumla.

Mambo hayo ni pamoja na ;-

1. BAADHI YA viongozi na Watawala ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara WAMEMILIKI na KUJIMILIKISHA raslimali ardhi bila kufuata taratibu stahiki za kisheria (Wametekeleza Uporaji wa Ardhi)

2. Mabaraza ya Ardhi ya Kata za (W) Ngara yanaongoza kwa vitendo vya rushwa katika usuluhishaji wa migogoro ya Ardhi. Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri wa Wilaya ya Ngara (DED – NGARA) fuatilia hili suala maana liko chini ya ofisi yako. Gharama za Kunyanyua Meza ya Baraza (kama wanavyoziita) Mara iwe Tsh 200,000/= Mara iwe Tsh 150,000/= *Toeni Miongozo inayoeleweka* wananchi wanaumia sana. Unakuta Ardhi ya mgogoro ni ya Hekari 16 yenye Thamani ya Zaidi ya Tsh 3,000,000/= kisheria Baraza la Kata linasuluhisha nini wakati mgogoro unakuwa nje ya uwezo wake kama siyo kutaka kumuibia mwananchi (Its Totally A Jurisdictional Error)

3. Wahamiaji Haramu (Raia kutoka nchi jirani) wanaongezeka Ngara kwa kukaribishwa na kupokelewa na Viongozi wa Mitaa, Wenyeviti wa Vitongoji na wanawatoza hela za viingilio na faini za kuingiza wake zao, wiki chache zilizopita ndani ya *Kijiji cha Magamba* kata ya Murusagamba (W) ilikuwepo Opereshini ya kuandika Majina ya Kila mwanamme mwenye Mke kutoka nje ya nchi. Faini ilikuwa ni Tsh 20,000/= kwa kila mmoja. Operation hiyo iliongozwa na Orodha kadhaa ya wenyeviti wa Vitongoji. Wananchi kwa kutokujua taratibu wakawa wanadai Risiti kwa kulipia Tsh 20,000/= yao wakasahau kama Haramu yao huliwa kiharamu. Mamlaka anzieni huko nimetoa CODE. 

4. Kuchelewa na kuzorota kwa mazoezi ya ULIPAJI FIDIA ndani ya Vijiji na Wananchi kwa MIRADI kama TEMBO NICKEL na NELSAP (W) NGARA *nyuma yake kuna VIGOGO WA WILAYA.* Mamlaka zinazohusika zifuatilieni Suala la Fidia kwa kata ya Muganza na Bugarama (Kwa Mradi wa Tembo Nickel) na Kata ya Rusumo (Kwa Mradi wa NELSAP)

5. *80% ya MADIWANI wa H/W NGARA* hawafahamu kwa upana madhara ya kuishi na Wahamiaji Haramu katika maeneo yao kutokana na kwamba wengi wao hawana elimu ya kutosha ya Uraia na Usalama wa Taifa letu (Wengi wao ni DARASA LA 7 tu) wakiongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri wa sasa. Mamlaka zinazohusika zitenge muda kuwapa elimu ya uraia na utaifa waheshimiwa hawa ili wasiojua utaifa na uraia wajue (hata kama ni dakika zao za nyongeza kwenye Ligi ya Udiwani wa 2020/2025)

6. 20% ya Wahamiaji Haramu Ngara wana Vitambulisho vya Mpiga Kura, Wana Familia na Kadi za Kliniki za Tanzania, Wana Namba za NIDA na wengine wanapambana kupata Vyeti vya Kuzaliwa, wana mashamba, *nikiiwaza Ngara ya Miaka 25 ijayo* roho inakosa amani,  nafsi inaufariji moyo na hatimaye moyo unarejesha matumaini na maisha yanaendelea. Inahuzunisha. (Chanzo cha Tatizo ; Madiwani wa Darasa la 7)

7. Ongezeko la Madaktari na Wauguzi Kada ya Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Ngara *bado halijakidhi mahitaji ya wananchi*, DMO – NGARA ikikupendeza tuma maombi tena kuomba watumishi waongezwe kwa wingi huku vijijini (hususani wahudumu wa kike). Hii itapanua wigo wa huduma na kuongeza kujiamini kwa wazazi wetu (mama zetu).

8. Shule za Misingi nyingi za Ngara hazina madawati. Kamati za Shule, Idara ya Elimu Msingi Kata na Wilaya (ikiwemo na Ofisi ya Mkurugenzi) wanaongeza nguvu kwenye ujenzi wa shule shikizi huku wanafunzi wakikalia vumbi kwa kukosa madawati. *Ingefaa sana* mngepunguza baadhi ya gharama kutoka kwenye ujenzi wa shule shikizi na kuongeza madawati kwa zile shule ambazo bado zina vyumba vya kutosha vya madarasa. Suala la Umbali wa Mtoto na Uhaba wa Madawati vinapaswa kufanyiwa tathmini ya kina. Kipindi cha Mitihani ni AIBU MNO. Nadhani walimu mtanielewa hapa.

9. Kuna DIWANI VITI MAALUMU WA NGARA ambaye AMEAJIRIWA na chama, na bado tena anautaka utumishi na uwakilishi at the same TIME. Wanawake wa Ngara UNGANENI JAMAANI kuna mambo mengine yanatia aibu sana na ni dharau. Kwamba hatuna watu wa kusimamia nafasi hiyo moja na kuiwakilisha kwa usahihi ??

10. Askari wa UHAMIAJI wa Ngara *hawajui kumtofautisha* Mwananchi wa Ngara asiyejua vema lugha ya KISWAHILI *dhidi ya* Mhamiaji Haramu (Raia wa Nchi Jirani). Hiyo imani inapaswa kuhuishwa inanyanyasa raia.

11. Kuna Mahusiano ya Kimapenzi Baina ya Madiwani ndani ya Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Ngara *kinyume na Maelekezo ya Kanuni za Madiwani*, hii hali ni hatarishi na haina afya kwa maamuzi bora yahusuyo MSTAKABARI wa Ngara yetu na uwakilishi wake. 

12. HADI sasa HAKUNA MAHUSIANO mazuri kati ya MAAFISA WA TAKUKURU (W) NGARA na WANANCHI. TAKUKURU (W) NGARA tembeleeni wananchi vijijini, Rushwa imetapakaa sana huko KULIKO UPENDO. Msikae Maofisini na kusubiria kukagua miradi ya umma tu.

13. KILA TAJIRI (Mwenye Mali) ndani ya Ngara *ana Kigogo wake Ndani ya watumishi, watawala na Viongozi wa Halmashauri ya Ngara*, mwananchi ukiteswa na KIGOGO wa Mtaa wako leta taarifa kamili na vielelezo kisha utuone sisi wazalendo wa Ngara tukusemee.

14. Mapori ya KEZA, na KASULO yanaongoza wilaya nzima ya Ngara kwa kuwa na Wachunga Ng’ombe ambao siyo RAIA wa TANZANIA. Uongozi wa Wafugaji (W) Ngara ingilieni kati. Usalama wa Raia wetu upeni kipaumbele kuliko mifugo yenu.

15. 60% ya WALIMU vijana ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Ngara *wana mahusiano ya SIRI ya Kimapenzi na Wanafunzi*. Idara ya Elimu Sekondari ongezeni umakini, walimu wasiwe chanzo cha kuua Confidence za watoto wetu na wadogo zetu mashuleni.

16. Maafisa MIFUGO wa Kata (W) Ngara wanaruhusu kuuzwa kwa Nyama yenye shida siku ya SOKO kwa RUSHWA isiyozidi Tsh 20,000/= AFISA MIFUGO wa Wilaya (kama upo) Murika Machinjio ya Soko la MUKUBU na MUKALINZI (Muganza), KEZA na MURUSAGAMBA. Ipo siku vitendo vya Rushwa vya Maafisa Mifugo vitatuulia ndugu zetu. 

17. 90% ya MADIWANI wa H/W Ngara wanaomiliki BAR, na GUEST HOUSES wameajiri WAHAMIAJI HARAMU kama watumishi wao, AFISA UHAMIAJI na OFISI YA DSO hawa waheshimiwa wanapaswa kuwajibishwa na kufanywa Mfano. Badala ya kuitetea Halmashauri dhidi ya Uvamizi wa Kigeni wana HALALISHA HARAMU. Mkitaka Codes nitawapatieni.

18. Watumishi wa Umma (Kada zaidi ya Moja) Tarafa ya Kanazi, na Murusagamba wanaongoza KULEWA mida ya Kazi (saa za kazi). Wasipobadilika nitakuja na PDF yao muda so mrefu, Afisa Utumishi (W) NGARA ukitaka Codes nitakupatia.

19. Wanaotoza USHURU wa Mazao kwenye BERRIERS za Mazao (W) Ngara hawajawahi kushiba pesa, ni RUSHWA mbele. Wanawaonea wakulima wanaotoka mashambani kuvuna hasa msimu huu wa Mpunga (hii inauma sana), na kuachia Magari (Maroli ya Mizigo) kwa vichenji na Receipts za bei ndogo (Hii hainihusu)

20. WAWEKEZAJI WOTE wa Mifugo (H/W) NGARA wana mawasiliano na Ofisi ya MKUU WA WILAYA : Kwa LOLOTE linalohusu MIFUGO, KERO, HUJUMA, PONGEZI ama MAFANIKIO, OFISI YA DC – NGARA *inapaswa kuhusishwa kwa Umuhimu*.

NINAOMBA KUWASILISHA NA NIKO TAYARI KUTOA USHIRIKIANO KWA KILA LILILOANDIKWA HAPO JUU (Ushirikiano ni kwa wenye Ofisi tu basi / Watawala)

🙏

By admin

Leave a Reply