MBUNGE WA NGARA AZUA GUMZO KUGAWA SIMU MOJA NA KOMPYUTA MOJA KWA KATA YA MABAWE

By Benny Bert Apr 14, 2025

Mbunge wa Jimbo la Ngara Mh. Ndaisaba George Ruhoro ameibua mjadala mkali kwa wananchi wa Jimbo la Ngara baada ya kukabidhi Kompyuta moja na Simu moja kwa kile alichodai ni kuchochea maendeleo ya Kata ya Mabawe. Kupitia chapisho aliloliweka kupitia Ukurasa wake wa Facebook, Mh. Ruhoro ameandika:

Nimetimiza ahadi ya kutoa Computer na Simu janja kwa Wananchi wa Mabawe. Computer inakwenda kutumika kufundishia wanafunzi wa Mabawe secondary mafunzo ya Computer kwa Vitendo. Mahitaji bado ni makubwa hivyo yeyote anaye wiwa tunamuomba aongezee.

Kupitia mijadala inayofanywa na wananchi mbalimbali wa Jimbo la Ngara inaonyesha wananchi kusikitishwa na tukio hili ambalo wananchi hao wanaona kama igizo la kisiasa ama dhihaka kwa wakazi wa Kata ya Mabawe.

Wananchi wanauliza ni kwa namna gani wanafunzi wa Shule ya Sekondari Mabawe wataweza kujifunza kwa kutumia Komputa moja? Lakini kwanini msafara ulioletwa kukabidhi mkataba unaonekana umetumia gharama kubwa ukilinganisha  na thamani ya kilichokabidhiwa?

Wananchi wengine wameenda mbele zaidi na kuhoji sababu ya msaada huu kutolewa wakati huu wa kuelekea uchaguzi mkuu?

Kwa ujumla tukio hili la Mbunge kugawa Komputa moja na simu moja limeibua malalamiko makubwa ya wananchi huku wakionyesha kuchukizwa na kile wanachokiita Maigixzo kutoka kwa Mbunge huyo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *