JOSIAS CHARLES AKOLEZA VITA YA UBUNGE NGARA.

By Benny Bert Apr 14, 2025
Ndugu Josias Charles

Kada maarufu wa Chama cha Mapinduzi kutoka Wilaya ya Ngara ndugu Josias Charles amekoleza Joto la  Ubunge katika Jimbo la Ngara baada ya kuweka Chapisho mtandaoni kuonyesha kutafakari maoni ya wananchi wanaomtaka kugombea nafasi hiyo ndani ya Jimbo la Ngara. Chapisho hili linakuja muda mfupi tuu baada ya Mbunge wa Ngara Mh. Ndaisaba Ruhoro kutangaza hadharani kuwa atagombea nafasi hiyo ya Ubunge kwa awamu nyingine.

Katika Chapisho hilo Josias Charles ameonyesha kuguswa na maoni ya wananchi wanaomtaka kujitokeza kugombea nafasi hiyo ya Uwakilishi katika Jimbo la Ngara. Chapisho hilo Josias Charles anasema:

Josias Charles ni nani haswa?

Josias Charles, Mtoto wa Pili katika familia ya Mzee Charles Isaya, akiwa amezaliwa mwaka 1992 katika familia ya wakulima wa kipato cha chini kabisa na kuanza elimu yake ya Msingi mnamo mwaka 2000 katika Shule ya Msingi Ngara Mjini, baadaye alihamishiwa Shule ya Msingi Nakatunga aliko maliza darasa la saba mwaka 2006. Josias Charles alichagulikuwa kujiunga na Shule ya Secondary Muyenzi iliyoko Tarafa ya Rulenge Wilayani Ngara ambako alisoma kidato cha kwanza mpaka kidato cha Pili na baadaye kuhamia Shule ya Ngara Secondary alikohitimu kidato cha nne mwaka 2010.

Josias Charles alichaguliwa kujiunga na kidato cha tano katika Shule ya Sekondari Rutabo iliyoko Kamachumu wilaya ya Muleba ambapo alihitimu kidato cha Sita mwezi February mwaka 2013. Baadaye mwezi October, 2013 Josias Charles alijiunga na masomo yake ya Shahada ya kwanza katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambako alisoma Shahada yake ya kwanza ya Ualimu akibobea katika Somo la Historia na Saikolijia ya Watoto. Josias Charles alihitimu Chuo Kikuu cha Dodoma mwaka 2016.

Baada ya kuhitimu Shahada yake ya kwanza aliendelea kujiendeleza katika mafunzo mbalimbali mpaka pale mwaka alipojiunga na Chuo cha Diplomasia kusoma Stashahada ya Uzamili katika Uhusiano wa Kimataifa (PGD In Management of Foreign Relations) ambako alihitimu mwaka 2022.

Mwaka 2024 Josias Charles alijiunga na Chuo Kikuu Huria kusoma Shahada ya Uzamili katika Uhusiano wa Kimataifa na Maendeleo ambayo anaendelea nayo mpaka hivi sasa.

Kwa kifupi Josias Charles ni kijana mpambanaji , mwenye misimamo na mpigania haki ambaye ana uzoefu mkubwa pia katika masuala ya Uongozi.

Je kauli ya Josias Charles kutafakari kuwatumikia wana Ngara inaweza kuwa na maana ya kuwa sasa Rasmi anafikilia kugombea nafasi ya Ubunge kwa Jimbo la Ngara? Hili ni swali ambalo mpaka sasa halijapata majibu japo Jitihada za mwandishi wetu kuzungumza naye kwa njia ya Simu  zimepata majibu mafupi. Josuias Charles alipopigiwa  Simu alijibu kwa ufupi kuwa

“Tujipe muda kuendelea kutafakari, Lolote linaweza kutokea kwani Sifa tunazo, Uwezo tunao na dhamira tunayo”

Baada ya andiko lile la Josias Charles katika Mitandao ya Kijamii maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Ngara kumekuwa na hisia mseto kuhusu endapo Josias Charles ataweza kupambana na vigogo wanaoonyesha dhamira ya Kugombea katika Jimbo hilo huku baadhi ya Wananchi wakionyesha kukubali uwezo wake wa Kujenga hoja huku wakionyesha wasi wasi kuhusu Kutokuwa na uwezo wa kifedha wa kushindana na wanasiasa wengine ambao wanagawa Rushwa kwa nguvu kubwa.

Sisi kama Ngara TV tunaendelea na jitihada mbalimbali kuendelea kukuhabarisha kuhusu mchakato wa Joto la Uchaguzi linaloendelea katika Wilaya ya Ngara. Usikae mbali na tovuti hii ya Ngara TV.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *