Ndugu Zangu Wana Ngara

By admin Mar 21, 2025

Na Sam Ruhuza

Ngara tunapitwa na mengi kwakuwa tunajipendekeza sana ccm, lakini haiwataki na ndio sababu hauwezi kumsikia Rais wala PM wanakuja na katika teuzi hausikii mwanangara, ila wao wapo bize kila kona kushangilia na kusema mitano tena! 

Inakera sana, Kilimanjaro, Arusha, Kigoma upinzani mkali kila siku Rais, Makamu, PM wanapishana na kila teuzi lazima utakutana na majina ya maeneo hayo! 

Ngara ukisema haya, wanakwambia Acha kuongea hivyo, Mama anafanya makubwa! 

Yaani woga wa kuongea mambo yanayotuhusu umepitiliza,lakini Rohoni watu wanaumia, ndio unafiki wenyewe huo! 

Ongea, Paza sauti usikike kama hiyo mikoa walivyopaza sauti kwenye chaguzi hadi wamesikika na kuambulia hayo! 

Mfano Kigoma mkoa mzima walipoikataa ccm, ili kurejesha imani imebidi Makamu Rais atoke huko, Gavana Benki Kuu, Wakurugenzi wenye maamuzi ya miradi ni kutoka Kigoma. Barabara za Lami, Umeme, Maji,.. miradi kibao viwanda vingi na hadi Bandari inajengwa, yaani wamefufuka baada ya kuikataa ccm na Waziri Mkuu ndio amepewa kuwa Mlezi wa Mkoa kila siku yupo Kigoma kusikiliza kero zao!! 

Huo ndio upinzani unaotakiwa toka kwa wananchi, Mtawala asiposikiliza hoja zenu, mnamkataa, kisha anakuja mbio kutekeleza, ila sisi Ngara waoga hata kujiongelea shida zetu, viongozi wetu wao kutwa ni kusifia tu, sijui kero zetu wanadhani nani wa kuzitatua! 

Ngara wanajua kubadilisha Wabunge na Madiwani, hao kwakuwa wanaishi nao, wanaona size yao,ila chama ni hicho hicho, tunatakiwa kushtuka kuona kwamba tunabadilisha Wabunge na Madiwani lakini bado hatuonekani, shida sio hao na Ukweli nawaelezeni shida yetu sio Mbunge wala Diwani bali ni ccm kama chama, wewe unaipenda sana ccm, baki nayo usitoke, ila kwa maslahi mapana ya Ngara mchague mgombea wa chama kingine, kisha muone mabadiliko! Utakuwa umeisaidia sana ccm kuamka kama ilivyo hiyo mikoa mingine!! 

Ipo siku mtakumbuka haya maneno! 

Ngara ni yetu sote Ndugu zangu, tuachane na uvyama na kuiweka Ngara mbele na kutoa adhabu kwa mtawala pale inapobidi tunapoona hatufaidi cake ya nchi kwasababu Ngara tunachangia pato la Taifa tena ukubwa wake kuna boda mbili kubwa ya Burundi na Rwanda/DRC Dola nyingi zinaingia. 

Vyuuka!! 

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *