Riport za CAG na TAKUKURU  

By admin Mar 29, 2025

Na Sam Ruhuza

Jana na leo nimefanya kujiridhisha tu uelewa wa wananchi kuhusu CAG na TAKUKURU Reports! 

Kwanza walio wengi hata hawakujua kama CAG na TAKUKURU Reports zinasomwa jana! 

Pili wengi hata hawakuelewa faida ya hizo Reports na zinataka nini?! 

Wengine wakanimaliza kabisa kwa kuhoji kama hizo Taasisi zinaongozwa na vyama vya upinzani! 

Katika moja ambayo yanampa usingizi mnono mtawala wala asijisumbue, ni uelewa wa wananchi kuhusu utendaji kazi wake Serikalini! Laiti Wananchi wangekuwa na ufahamu hata kidogo, basi mtawala angekuwa makini sana. 

Unaangalia TV na Radio wapo bize na uchambuzi wa michezo pamoja kupigia debe wagombea wao uchaguzi lakini mijadala hii ya uchumi wa nchi, hakuna nafasi na inatolewa na vyombo vichache sana! 

Ninachoogopa ni siku hawa Wananchi wakiamka ghafla na kujitambua, mambo mengine yatakuwa history! Kila mara nasema humu, anayekutahadharisha jambo ama kukukosoa anakupenda zaidi ulete mabadiliko kuliko yule anayekusifia na kukuabudu muda wote akiwa analinda maslahi yake! 

Hivi unafikiri hao wanaosababisha hasara kubwa Serikalini wakiwa wanaongea na wananchi wanakuwa wanaongea nini zaidi ya kusema lugha ya ‘anaupiga mwingi’, ‘mitano tena’, halafu mtawala anafuraaahi na kumuona ni mtu wake, kumbe yupo kimaslahi zaidi! 

(203) 🤔CAG: KUNA HATARI YA MKOPO KUTOREJESHWA🙆🔥 #breaking #globaltv #shortsvideo #viralvideo #trending – YouTube

Ukiona watu kuabudu sana mtawala, jiulize, Kulikoni??!!  

Leo March taarifa ya Mwaka 2023 CAG na TAKUKURU inakabidhiwa kwa Mheshimiwa Rais, kisha mjadala Bungeni utafanyika Bungeni baada ya miezi 6, na hivi itakuwa uchaguzi mkuu, hiyo ni hadi mwaka kesho tena hata habari imepoa!! 

Kitu kingine ni kwamba hizi taarifa hazina nguvu yoyote zaidi ya kukujenga hasira za muda tu kuona baadhi ya maeneo mabovu, lakini baada ya hapo hakuna kusikia mabadiliko zaidi ya Reports zinazofuata kuja kuyasikia yaleyale! 

Serikali imekuwa ikishauriwa sana kubana matumizi, lakini hilo limewashinda hadi CAG ameona mabilioni yasiyo na tija! 

Mtumishi anatakiwa atambue pesa ya Serikali ni kama pesa yake, awe na uchungu nayo, aidhibiti na sio kuitumia hovyo! 

Serikali sio Mfanyabiashara, mfano TRC, Serikali ijenge Reli SGR kama ilivyofanya, lakini kuendesha wapatie sekta binafsi kama ilivyo Barabara, Serikali inajenga Barabara lakini magari ni watu, hivyohivyo kwenye reli inatoa huduma za njia na vituo lakini Uendeshaji sio wao, hapo hasara hakuna. 

Ndege hivyohivyo na mashirika mengine.  

Naelewa kuna mashirika lengo ni kutoa huduma bila faida na usalama, basi Serikali iwe na ubunifu wa kupunguza hiyo hasara.  

Hiyo hasara ya Shirika, Serikali ni hasara yetu wananchi kuibeba. 

Hao Wakurugenzi wa mashirika ya umma waombe kazi na kupitishwa kwa sifa zao pia mikataba yao ilindwe na sio uteuzi na utenguzi kila kukicha haina tija yoyote.  

Bado mashirika yetu yanaendeshwa kisiasa sana hata teuzi zao kuanzia bodi zimekaa kiushikaji zaidi ya sifa. 

Kuna mengi ya kuangalia kwenye utendaji wa pesa za umma kuondoa huu upotevu! 

Tanzania ni yetu sote! 🇹🇿🤝

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *