KUDHIBITI RUSHWA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU, MIKUSANYIKO KWENYE “KUMBI BUBU” JIMBO LA NGARA IDHIBITIWE.
Na: Josias Charles
Wakati nikiwa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) nilikuwa mwanachama wa Club ya Kupambana na Rushwa (PCCB Club). Huko tulifundishwa mambo mengi sana ya Uzalendo na kubwa zaidi likiwa kuhusu kudhibiti na Kupambana na Rushwa.Â
Kwa kutumia ujuzi niliopata ninawajibika kukemea rushwa na kutoa taarifa ama tahadhali kuhusu viashiria vya Rushwa kwenye jamii.
Ninavyoandika hapa kuna ninaibua mashaka yangu kuhusu ukumbi unaomilikiwa na Mbunge wa Jimbo la Ngara na ulioko nyumbani kwake ambao umekuwa ukitumika kukusanya Wajumbe/Viongozi wa Chama na hata wananchi wa Kawaida kinyume na utaratibu.
Maswali yanayoibuka ni Je Ukumbi huu umesajiliwa na una Vibali kutoka Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)?
Je Matukio yote na Mikusanyiko yote inayofanyika kwenye ukumbi huu wenye ulinzi mkali inapata Vibali kutoka kwenye mamlaka za Serikali?
Je shughuli zinazofanyika kwenye ukumbi huo mara kadhaa ikiwemo kugawa fedha, Mchele na Mafuta ya Kupika kwa watu wanaotarajiwa kuwa wapiga kura kwenye chaguzi zijazo vinafanyika kwa malengo yapi?
Je ni sababu zipi zinapelekea watu kunyang’anywa simu zao wakiwa kwenye geti la kuingia eneo hilo? Kama shughuli zinazofanyika humo ni halali, kwanini watu wanany’ang’anywa simu zao na kufanyiwa upekuzi mkali?
Kuruhusiwa kwa vitendo hivi kunachochea Rushwa na kunaondoa dhana ya “Uwanja sawa katika Kushiriki shughuli za Kisiasa”.
Imeazimwa kutoka Simamiatv: Habari Kamili, gusa maandishi ya blue
Baada ya ujumbe huu, ninaomba mamlaka zote za Serikali zisimame kidete kusimamia shughuli zinazoendeshwa katika ukumbi huo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa kila tukio lina kibali na shughuli zinazofanyika humo zinakuwa na uwazi na sio kwa uficho kwa kiwango cha kunyang’anya simu na upekuzi mkali kwa watu wanaaoitwa kwenye ukumbi huo.
Mwisho kabisa, Nitoe rai kwa kila mwana Ngara kusimama kidete kukataa Rushwa kuelekea uchaguzi mkuu….. Matumizi ya Rushwa ndiyo yanatulrta Viongozi ambao wako busy na “Uchifu” badala ya kuwa busy na kusemea kero za Wananchi kama vile ubovu wa Stand ya Ngara nk.