Siasa: Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Antiphas Lissu akamatwa na Jeshi la Polisi RUVUMA

By Titho Philemon Apr 9, 2025

Jeshi la Polisi Mkoani Ruvuma limepiga mabomu na kumkamata Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Ndugu Tundu Antiphas Lissu muda mfupi baada ya kumaliza kuhutubia mkutano wake huko Mbamba Bay, Wilaya ya Mbinga Mkoani Ruvuma.

Tukio hilo limetokea leo Jumatano ya April 9, 2025 katika eneo la Mbamba Bay Mkoani humo.

Aidha, Askari Polisi wamemvamia na kulazimisha kumkamata huku wakipiga mabovu ya machozi kuwatawanya wananchi pamoja na wanachama wa CHADEMA waliokuwa wamehudhuria mkutano wake ili kurahisisha ukamataji wake. Wananchi na wanachama wa CHADEMA wamesambaa baada ya kuzuka kwa taharuki hiyo huku wakiwa na sintofahamu ya kutokujua sababu za kukamatwa kwa kiongozi huyo Mkuu wa chama kikuu cha pinzani nchini huku mahali anakopelekwa kukiwa hakujawekwa wazi.

Ngaratv.com itakupatia taarifa za ziada kuhusu tukio hilo pale zitakazopatikana.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *