Sifa za Mbunge Mpya wa Jimbo la Ngara

By admin May 12, 2025

 

Ni mara chache sana kukuta Wananchi wakizungumza kwa uhuru kujisu kiongozi hasa Mbunge wamtakae,kwasababu wengi wanaochaguliwa wanafanikisha malengo kwakutumia Pesa!

Leo, kidogo tu niliongelee jimbo langu mama la Ngara,jimbo tajiri na lenye rasilimali kibaaao!

Oktoba mwaka huu tutafanya Uchaguzi mkuu kuwapata viobgozi keaajili ya kutuvusha kimaendeleo kwa mkataba wa miaka 5. Rais,Wabunge na Madiwani. 

Ili Rais kama kiongozi mkuu wa Nchi atekeleze ahadi za Wananchi qnahitaji kupata ushirikiano wa viongozi wenzake. Kiungo kati ya Diwani na Rais ni mheshiniwa Mbunge. Kwa maana hiyo, Wananchi wa Jimbo la Ngara wanahitaji kuchagua Mbubge Bora,sio Bora Mbubge mwenye sifa zifuatazo.

1. UHUSIANO WA KARIBU NA WANANCHI

Mbunge anayetakiwa lazima awe na uhusiano wa karibu na wananchi wa jimbo lake. Hii inajumuisha kujua na kuelewa changamoto zinazowakabili wananchi na kuwa na uwezo wa kuwasiliana nao kwa ufanisi. Mbunge anapaswa pia kuwa na uwezo wa kueleza matatizo ya wananchi na kuyapeleka kwenye mamlaka husika ili kupata suluhisho .

2. AWE BA UWEZO BINAFSI WA KULETA MAENDELEO ENDELEVU

Mbunge anayetakiwa lazima awe na uwezo wa kutafuta na kuleta miradi ya maendeleo inayohitajika katika jimbo lake. Hii inajumuisha kutafuta rasilimali na kushirikiana na serikali na wadau mbalimbali ili kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

3.UWEZO WA KUWAUNGANISHA WANANCHI

Ngara, inahitaji Mbunge mwenye uwezo wa kuwaunganisha wananchi wa jimbo lake ili kushirikiana katika shughuli za maendeleo. Hii inajumuisha kuhamasisha ushirikiano kati ya wananchi, viongozi wa serikali na wadau wengine ili kufanikisha malengo ya maendeleo.

4.UWEZO NA MSIMAMO

Mbunge anayetakiwa lazima awe na msimamo thabiti katika masuala ya kitaifa na kimataifa. Hii inajumuisha kuwa na uelewa wa kina wa masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii na kuwa na uwezo wa kutoa maoni na mapendekezo yenye tija kwa maendeleo ya jimbo lake na taifa kwa ujumla.

5.MBUBGE MWENYE KUSIMAMIA NA KUONGOZA KWA KUFUATA UTAWALA BORA 

Mbunge anayetakiwa lazima awe na uwezo wa kuwa kiongozi bora ambaye anaweza kuongoza kwa mfano. Hii inajumuisha kuwa na maadili mema, uaminifu, uwazi na uwezo wa kufanya maamuzi sahihi kwa manufaa ya wananchi wa jimbo lake.

Ni muda muafaka wa kila mwananchi kuanza kufanya utafiti wa Mbunge anaefaa.

Je,  wewe utamchagua nani?

By admin

Leave a Reply