Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) ndani ya wilaya ya Ngara ni Moja kati ya mamlaka za kiutendaji ambazo uwajibikaji wake unapaswa kutiliwa shaka. Haki ya Kupata Vitambulisho vya Taifa ambayo ni haki ya kila Mtanzania wa kuanzia umri wa miaka 18 na kuendelea imekuwa haitolewi na kupatikani ipasavyo!
Wananchi wengi wamekuwa wakipitishwa kwenye msururu wa taratibu na zingine zisizo rahisi na hatimaye kuwapelekea watanzani hao wazawa wakikosa NIDA huku raia wengi wa kigeni wenye pesa na connections huku uraiani wakionekana kuwa na NIDA. Hii ni aibu sana kwa wilaya na taifa na Maafisa wa NIDA Ngara wanapaswa kukaguliwa (Internal Assessment) na wale watakaobainika kuhusika na ucheleweshwaji huu pamoja na tabia za kuwasajili raia wa kigeni kwa michongo wachukuliwe hatua stahiki za kisheria.
NGARA KWASASA:-
- Kama ni mtu mzima na haujasoma hauwezi kupata kadi wala namba ya NIDA kwasababu utaombwa uambatanishe cheti cha kuzaliwa na cha darasa la Saba (wengi wana kadi za kliniki tu hawana vyeti vya Kuzaliwa na wengine hata darasa la nne hawajafika /cheti cha shule hana), Je NIDA Ngara wanataka tuamini kwamba bila cheti cha darasa la saba hauwezi kupata Namba ya NIDA ?
- Raia wa Kigeni (Mrundi, Mnyarwanda n.k) akiwa na pesa ni vyepesi sana kupata NIDA tena kwa siku chache na wengine kwa masaa tu huku WATANZANIA (wazawa) wakipata mlolongo Mkubwa na wengine kupuuzwa licha ya mwendo mrefu wanaoutembea kufuata huduma hiyo wilayani, inahuzunisha sana!
- Utaratibu wa Muombaji wa NIDA kutambulishwa na uongozi wake wa serikali za Mitaa hauna nguvu kama Sheria na Miongozo inavyotaka. Jamii inahamu na shauku kubwa kujua, Je kuna shida gani kwa NIDA – NGARA kuweka bayana taratibu za kupata namba ya NIDA bila vikwazo na bila kupoteza muda na gharama kubwa? Maana hakuna busara ya kiutendaji kuona Kijana wa Kata kama Murusagamba, Muganza na Bugarama kukesha barabarani mara mbili kwa wiki (Twice a week) wakati uwezekano wa kuweka mchakato huo wazi upo na upo ndani ya majukumu ya NIDA Ngara?
OMBI LANGU KWA NIDA NGARA
- Wahakikishe Kila Muombaji aliyekidhi vigezo anasajiliwa kwa ueledi na hatimaye apate namba yake ya NIDA. Siafiki sana zoezi lenu la kuja kusajili NIDA vijijini bila ueledi kwakuwa mnawapima watu kwa mionekano kwamba wewe ni mdogo haujakua huku NIDA wakiwa na haraka ya kumaliza kazi na kuwahi kwenda Ngara bila kumaliza zoezi hata kwa 75%
- NIDA – NGARA wajitahidi kuwa na hekima katika kufuatilia na kuchunguza uhalali wa uraia katika kutekeleza jukumu lao hilo la kikazi na kitaaluma.
- NIDA – NGARA wekeni mipaka ya kiutendaji ili viongozi wa kisiasa wasiwe na Nguvu ya kuingilia mamlaka yenu kama hali ilivyo kwasasa. Nasema hivi kwasababu kuna sehemu Katibu wa CCM wa kata alikuwa anamconnect mwananchi na Afisa wa NIDA ili aweze kumpa hela amsaidie kwa haraka. Hii haina afya kiutendaji.
NIDA NGARA BADILIKENI, JENGENI IMANI UPYA, TOENI ELIMU KWA WANANCHI, KISHA WATUMIKIENI.
NGARA, AMANI NA MAENDELEO!
💪💪💪🤲🧎♂️🙏