Ruhoro: Si Msamalia, Bali Mlubuni

By admin Sep 18, 2024
Bibiana Kagaigai akikanusha kusomeshwa na Mheshimiwa George Ruhoro; Adai nia kubwa ya Ruhoro ilikua ni kumrubuni nakupata ukaribu na famili ya Kagaigai. Ruhoro amekua na kiu cha kuwa mlinzi wa familia za wana Ngara na pengine juhudi za kumtunza mwana Kagaigai kumefunua hali ya joto la kisiasa inayomnyima amani Wilayani Ngara.

Jana, tarehe 17 mwezi wa September mwaka 2024 ujumbe ulisambazwa kwenye magroup mbali mbali mitandaoni iliyopo whats app. Ujumbe uliosambazwa mitandaoni ulielezea jinsi Mheshimiwa Ruhoro, Mbunge wa Jimbo la Ngara, alivyosaidia mmoja wa familia ya kwa Kagaigai kwa kumlipia ada za shule baada ya kutelekezwa na ukoo wa Kagaigai. Ujumbe uliosambazwa mitandaoni ulisifia ukalimu na usamalia wa ndugu Ruhoro ambapo mbunge huyu amekua anapepea kwenye vyombo vya habari kwa kujaribu kutunza familia za watu wengine hususani familia za watemi wa kimila Wilayani Ngara. Kitaifa, miaka kadhaa iliyopita, agizo la Mheshimiwa George Ruhoro kwa wakazi wa Ngara eti watundike picha yake majumbani kwao liligeuka gumzo kwa watanzania wengi.

Mheshimiwa Ruhoro anatarajia kumalizia muhura wake wa Kibunge wa kuwakilisha Wilaya ya Ngara kwenye Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ruhoro anatarajia kutetea na kuomba wana Ngara apewe muhura mwingine wa kuwakilisha Jimbo la Ngara Bungeni.

Wiki kadhaa zilizopita mtandao wa Simamia.com ulitoa orodha ya wanaotarajia kutia nia ya kugombea nafasi ya ubunge mwaka 2025. Mmoja ya walio orodheshwa kama watia nia ya kugombea ubunge kupita Jimbo la Ngara ni Steven Kagaigai. Steven Kagaigai amekua ni mzalendo na ni mtu wa Ngara ambaye amelitumikia Taifa lake kikamilifu na moja ya nafasi alizowahi ni kutumikia ni kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kutokana na uchunguzi uliofanywa na Gazeti la Ngaratv.com, Steve Kagaigai ni moja ya watia nia wenye ushawishi mkubwa Wilayani na wenye uwezo kumtua ubunge Mheshimiwa George Ruhoro ambaye anamalizia miezi saba iliyobaki kwenye uwakilishaji wa Jimbo la Ngara Bungeni. Joto la Siasa, na kile wapambe wa Ruhoro wanaokiita usamalia umeperekea George Ruhoro kujaribu kuwa mtemi wa watemi wa kimila wilayani Ngara, kipenzi-ng’ang’anizi kwa wale waliobandika picha yake nyumbani kwao na jana msamalia mwema anayedai kusaidia kusomesha mmoja wa familia kutoka kwa Kagaigai. Mheshimiwa Ruhoro huyo huyo amekua akikubwa na kashfa kutoka kwa wanawake mbali mbali ambao wanadai kuzalishwa na kisha kutelekezwa bila kupewa huduma ya kutunza watoto.

Aliyetajwa kunufaika na usamalia wa Mheshimiwa Ruhoro ni Bibiana Kagaigai. Bibiana Kagaigai amekili kusogelewa na kulubuniwa na Ruhoro. Kwa risiti kutoka Benki, Bibiana amethibisha kulipiwa gharama za shule na familia ya Kagaigai na kukanusha kile Ruhoro na wapambe wake wanachojaribu kuaminisha jamii.

Bibiana akiwa mbele ya kamera za simamiatv, gusa maandishi ya bluu kuona video, ameomba serikali impatie ulinzi kutokana matukio yanayotokana na wimbi la kisiasa linaloendelea. Bibiana amekanusha madai juu ya Ruhoro kumlipia ada ama gharama zozote zinazohusiana na safari yake ya kimasomo.

Video imeazimwa kutoka SimamiaTV: Link:

BIBIANA AKANUSHA TAARIFA YA KUTISHIWA KUULIWA NA BABA YAKE MKUBWA STEVEN KAGAIGAI (youtube.com)

Na ujumbe uliosambaa na kusifia kile kilichoitwa usamalia wa George Ruhoro uliofikia gazeti la Ngaratv.com kwa njia ya What’s App:

*HABARI MBAYA KWA WANANGARA!*

*HOFU YA USALAMA KWA “BIBIANA WILSON KAGAIGAI”📍*

Habari kwa Ufupi!

“Bibiana Wilson Kagaigai” ni mtoto wa mdogo wake na Steven KAGAIGAI aitwaye Wilson KAGAIGAI.

Wilson Kagaigai na Mke wake walitengana na kuwatekekeza watoto wao pale MUHWEZA kwa bibi yao yaani mke wa Steven KAGAIGAI.

Bibiana KAGAIGAI alifaulu kwenda Advance huku wadogo zake wakiendelea kupata elimu yao ya sekondari pale MABAWE SEKONDARI.

Bibiana *alimuomba msaada* baba yake mkubwa STEVEN KAGAIGAI ili amsomeshe lakini hakumsomesha na hivyo bibiana akakosa msaada.

Baada ya wasamalia kuona akili na umakini alionao Binti Bibiana waliamua kumpeleka kwa Mr. Ruhoro na yeye kwa roho yake nzuri na ya kujali utu akaamua kumsaidia na kuwa sehemu ya faraja yake katika safari yake ya elimu.

Ukweli ulioko wazi ni kwamba Mheshimiwa Ruhoro alimlipia Bibiana ada zote za shule kwa maana ya Form 5 & 6 pale Mchungaji mwema sekondari *isipokuwa* ada ya Muhula wa Mwisho tu ambayo ililipwa na Ndugu yake mwengine.

Hadi muda huu mdada *Bibiana Wilson KAGAIGAI* anasubiria kwenda UNIVERSITY.

Wadogo zake na BIBIANA walikuwa wakisaidiwa na Mbunge huyu huyu Ruhoro kiasi cha kuwapelekea chakula pale nyumbani, na Mheshimiwa Mbunge amekuwa mkimya katika hili. Hakika ana roho ya utu sana huyu mbaba.

Ila baada ya Steven KAGAIGAI kutangaza na kuanza kufanya kampeni zake ndani ya Ngara, Mbunge RUHORO aliacha kwenda Nyumbani huku akiamini kuwa angewasaidia. Baadae wadogo zake Bibian wameacha shule na haijulikani walikokwenda.

Sasa Taarifa za BIBIAN kusomeshwa na Mbunge zimeifikia familia ya KAGAIGAI.

Baada ya kumaliza Form 6 Mdada Bibian anaishi kwa Mtu baki pale Ngara Mjini na hawezi KUFIKIA kwa KAGAIGAI.

Baada ya taarifa kumfikia KAGAIGAI huyo mtoto ametishiwa kuuliwa na maisha yake yako hatarini.

Meseji aliyowaandikia wanafunzi waliyesoma naye inaonyesha kwamba muda wowote anaweza kuuliwa na iwapo itatokea hiyo *mhusika wa moja kwa moja* atakuwa Steven Kagaigai na mke wake.

Kama msamaria mwema, *niliyeguswa na hali ya Binti Bibian* ninaziomba mamlaka za kiserikali zifanye haraka sana kujua baba wa watoto yuko wapi, mama wa watoto yuko wapi, na wadogo zake Bibian wako wapi *lakini zaidi* mamlaka zimlinde huyo Binti ili asiguswe wala kudhurika kwa lolote.

Mimi ni mmama ambaye ninajua uchungu wa watoto na kama mwanajamii naumia sana hasa nikiwaza kuvaa kiatu alichokivaa Bibian kwa sasa.

Serikali tunaomba mtusaidie katika hili.

Ndimi,

Msamalia Mwema kutoka Samalia.

Je wewe uliyosoma makala hii una lipi la kuongezea ama la kuchangia?

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *