ENGLAND YANYAKUA NAFASI YA TATU KWA KUICHAPA UFARANSA 6-4

By Na Mwandishi Jul 18, 2026

Na Juventus Juvenary-Ngara

Saa chache kuelekea Fainali ya Kombe la Dunia, Timu ya taifa ya England imehitimisha kampeni yake kwa mwaka huu 2026 kwa kutwaa nafasi ya tatu baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 6-4 dhidi ya Ufaransa katika mchezo wa kusaka medali ya shaba uliochezwa Julai 18, 2026.

Nyota wa mchezo alikuwa Bukayo Saka aliyefunga mabao matatu (hat-trick), huku Declan Rice, Ezri Konsa na Jude Bellingham wakiongeza bao moja kila mmoja.

Kwa upande wa Ufaransa, Kylian Mbappé amefunga mabao mawili, wakati Bradley Barcola na Ousmane Dembélé wakiongeza bao moja kila mmoja.

England imemaliza kipindi cha kwanza ikiwa mbele kwa mabao 4-0, lakini Ufaransa ikafanikiwa kurejea kwa nguvu kipindi cha pili na kupunguza tofauti kabla ya England kufunga mabao mawili ya mwisho na kuhitimisha mchezo kwa ushindi wa mabao 6-4.

Mbali na kuisaidia Ufaransa kufunga mabao mawili, mshambuliaji Kylian Mbappé ameandika historia mpya kwa kufikisha jumla ya mabao 22 katika fainali za Kombe la Dunia, na hivyo kumpita Lionel Messi aliyekuwa na mabao 21 katika rekodi ya muda wote ya mashindano hayo.

Wafuatiliaji wa Soka wanasema huenda Messi akapindua Messi na kuongeza idadi ya mabao iwapo atafunga katika fainali dhidi ya Hispania.

Ni suala la kusubiri. Tunakaribisha maoni yako msomaji. Hii ni www.ngaratv.com.

Tukutane baadae kwenye mtanange wa fainali…..Argentina dhidi ya Hispania.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *