Dotto Bahemu Aahidi Kushirikiana Na Rulenge AMCOS Kuwainua Wakulima Tarafa Ya Rulenge

By Na Mwandishi Aug 7, 2026

Mbunge wa Jimbo la Ngara, Mhe. Dotto Jasson Bahemu, amesema ataendelea kushirikiana na Chama Cha Ushirika cha Msingi cha Rulenge Amcos, kuwainua Wakulima wa zao la Kahawa katika Tarafa ya Rulenge.

Mhe. Dotto ameyasema hayo alipotembelea Makao Makuu ya Chama hicho, kinachojumuisha Wakulima wa zao la Kahawa katika kata ya Rulenge.

Amesema akiwa Mwakilishi wa Wananchi wa Jimbo la Ngara, atatumia nafasi hiyo kusimama upande wa Wakulima kwa ajili ya kutetea maslahi yao, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Wakulima wanagawiwa miche ya kutosha, pamoja na kuunganisha Chama hicho cha Msingi na Mamlaka za Kiserikali kupitia Wizara ya Kilimo, ili kuondoa changamoto mbalimbali ambazo zitabainika kuzikabili pande hizo mbili.

Awali akitoa taarifa ya Rulenge Amcos, Mwenyekiti wa Bodi ya Chama hicho Eng. Deusdedith Kakoko, amempongeza Mhe. Dotto Jasson Bahemu kwa jinsi ambavyo alishiriki kikamilifu katika Uzinduzi wake, pamoja na namna ambavyo ameonyesha nia ya dhati ya kuwasemea Wakulima wa zao la Kahawa katika wilaya ya Ngara.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *