
Na Juventus Juvenary Illambona-Ngara
08/08/2026
Kampuni ya bora na viwango inayohusika na zao la Kahawa Rukundoo Coffee Traders imewatakia wakulima na Watanzania wote kwa ujumla Heri ya Sikukuu ya Nane Nane, huku ikisisitiza umuhimu wa kuthamini mchango wa mkulima katika ujenzi wa uchumi wa familia, jamii na Taifa.
Akizungumza na www.ngaratv.com kwa niaba ya Rukundoo Coffee Traders, mmoja wa Wakurugenzi wa kampuni hiyo, Pendo Dan, amesema kampuni inaendelea kuthamini mchango wa wakulima na wadau wa zao la kahawa, ambao ndiyo msingi wa mnyororo wa thamani wa zao hilo.
“Ewe mkulima, popote pale ulipo, pokea salamu za upendo, pongezi na shukrani zetu. Tunatambua kazi kubwa unayoifanya katika uzalishaji wa kahawa na kujenga uchumi wa nchi yetu,” amesema Pendo Dan.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Nuru Christopher Nzoya amesema Rukundoo Coffee Traders itaendelea kuwahudumia wafanyabiashara na wadau wa zao la kahawa, huku kampuni ikiwa na makao yake Ngara, Mbinga na Dar es Salaam.
“Kwa wafanyabiashara wa zao la kahawa ambao mmewahi kupata huduma kutoka kwetu na wale tunaoendelea kuwahudumia, tunawaahidi kuendelea kutoa huduma bora.
Tumedhamiria, na nia tunayo,” amesema Nuru Christopher Nzoya.
Wakurugenzi hao wamewatakia wakulima wote nchini mafanikio mema, mavuno bora na tija katika shughuli zao za kilimo, wakisisitiza umuhimu wa kuendelea kuthamini kilimo na kumheshimu mkulima.
Rukundoo Coffee Traders inaungana na Watanzania wote kusherehekea Sikukuu ya Nane Nane.
