
Na Juventus Juvenary-Ngara
NGARA: Rukundoo Coffee Traders imeshiriki Mahafali ya 27 ya Shule ya Msingi Nyarusange, Kata ya Kanazi, Wilaya ya Ngara, na kutoa zawadi kwa wahitimu 67 wa Darasa la Saba pamoja na misaada kwa shule.
Kampuni hiyo, iliyowakilishwa na Mkurugenzi Mtendaji Bw. Nuru Christopher Nzoya kwa niaba ya Mkurugenzi Mwenzako Bw. Wilson Dan Nathanael, maarufu PENDO, iliwapongeza wahitimu na kuwapatia zawadi za kuhamasisha kuendelea na masomo kwa bidii.
Pia ilikabidhi mipira miwili, mifuko 20 ya saruji, pipa la kuhifadhia maji, na Computer 1 ( Desk Top) huku ikiahidi kuendelea kushirikiana na shule kutatua changamoto zake.



Akisoma risala, Mkuu wa shule Brighton Lazaro Mbanguka alisema shule inakabiliwa na uchakavu wa Chumba cha Darasa la Kwanza, upungufu wa vyumba viwili vya madarasa, ukosefu wa vifaa vya kuhifadhia maji, vifaa vya malazi kwa wasimamizi wa mitihani ya kitaifa na kompyuta za kuchakata taarifa na mitihani ya wanafunzi.
Bw. Nzoya alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya shule, wazazi, walezi na wadau katika kuboresha mazingira ya kujifunzia.
Aliwakabidhi zawadi wahitimu na wanafunzi walioshiriki michezo, na kuwataka wazazi kuwaandaa mapema watoto wao kwa hatua inayofuata ya elimu, hususan watakaoanza sekondari Januari 2027.
Ushiriki wa Rukundoo Coffee Traders umeonesha umuhimu wa mchango wa sekta binafsi katika kuboresha miundombinu, mazingira ya kujifunzia na ustawi wa wanafunzi.
