Siasa Sio Ugomvi

By admin Jul 23, 2025

‎Habari za asubuhi ndugu zangu wana Ngara! Japo wengine tukiandika tunatafsirika vingine,na wakati mwingine kuchochea hali ya kutopendwa na kuchukiwa zaidi, ila wazungu walituambukiza msemo “The truth will set you free”.

‎Kuanzia vitabuni na hata uzoefu kwa watangulizi wetu “Siasa siyo ugomvi wala uadui” Siasa safi ni ile  ya busara sana.

‎Kwa lugha nyingine,tunaweza kusema Siasa ni chombo cha kuwahudumia watu, lakini baadhi ya wanasiasa huchukulia kama njia ya kujinufaisha, hata kwa gharama ya kuvuruga amani, kueneza chuki, au kulazimisha ushindi kwa hila.

‎Hiyo ni mbaya sana ndugu zangu.

‎Tumefika hatua watu fulani kwa maslahi yao “Kulazimisha watu wao kushinda, kutumia pesa kuhonga na kuaminisha kuwa bila wao siasa haipo!” hali ni mbaya zaidi.

‎Binafsi ni seme tu,huko ndiko kiini cha ufisadi wa kisiasa. Ni aina ya uongozi wa kimaslahi binafsi — ambao hausitahili kupewa nafasi hapa Ngara,Kagera na Tanzania kwa Ujumla.

‎Jana wakati napitia taarifa mitandaoni nilikutana na neno WAFILISTI! Ni neno hilo ambalo lilinirudisha miaka mingi nyuma nikaukumbuka wimbo wa SAMSON & DELIRA “Wafilisti” walimdanganya Mke wa Samson,akambembeleza mme wake mpenzi akatoboa Siri ya nguvu zake hali iliyopelekea mateso makubwa na kutobolewa macho!.

‎Ni katika kipindi hikihiki kuelekea Uchaguzi mkuu tunapowashuhudia watu kwa maslahi yao binafsi wakiwagawanya wana Ngara, ilimradi tu watimize mahitaji yao/kushinda nafasi wazitakazo bila kupima athari na matokeo kwa Wananchi! Tabia za kifikisti hizi,hazifai.

‎Uchonganishi mwingi, ufitinishi mwingi , visa na mikasa kibao na mambo mengi ya ajabu kila kukicha!!!

‎Ni muda muafaka wana Ngara tuamue kwa pamoja kukemea tabia mbaya ya watu wanaotaka madaraka kwa nguvu na Hila. Wale wanaofikiri wao pekee ndio wanaofaa, au wanaojifikiria kuwa “mwisho wa mjadala” — watu wanaopotosha misingi ya demokrasia na usawa hawatufai. 

‎Nawatakia adubuhi njema.

‎Juventus Juvenary Illambona 

‎Mwanachama,CCM

‎Buhororo-Kibimba.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *