Anachokipigania Askofu Gwajima Ni Ukweli na Haki

By admin Jun 3, 2025

‎ANACHOKIPIGANIA ASKOFU GWAJIMA NI UKOMBOZI WA KWELI KWA TANZANIA” – WANANCHI NGARA

‎Na Mwandishi Wetu – Ngara

‎Wananchi wa Wilaya ya Ngara wameeleza pongezi zao kwa Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima, Dkt. Josephat Gwajima, kwa kuwa mmoja wa viongozi wachache wanaothubutu kusimamia haki za Watanzania bila kuogopa.

‎Katika salamu zao za wazi, wananchi hao wameeleza kuwa sauti ya Askofu Gwajima ni ya ukombozi, hasa katika nyakati ambapo baadhi ya viongozi wa serikali na vyama wamekuwa wakituhumiwa kwa vitendo vya kuvunja haki za binadamu.

‎“Askofu Gwajima ni sauti ya wanyonge. Anasimama mbele kupinga utekaji, kupotea kwa watu wasio na hatia, na kubeba kilio cha Watanzania waliochoka kunyanyaswa,” alisema kijana mmoja kutoka Rulenge.

‎Pongezi kwa Msimamo Wake Thabiti

‎Wananchi wamesema kuwa licha ya changamoto na upinzani anaokumbana nao, Gwajima ameendelea kuonesha uthubutu wa kuikosoa serikali na kulinda Katiba ya nchi kwa vitendo, si kwa maneno tu.

‎“Tunampongeza kwa kusema ukweli. Taifa linahitaji viongozi wa kiroho wenye ujasiri wa kusema kile ambacho wengine wanaogopa,” aliongeza mkazi mwingine wa Kasulo.

‎”Tuna jambo la kujifunza kutoka kwa Gwajima” anasema kijana wa Kanazi.

‎Wito kwa Viongozi Wengine

‎Katika ujumbe wao, wananchi hao wametoa wito kwa viongozi wengine wa dini, siasa, na taasisi za kiraia kuungana katika kutetea maslahi ya taifa na kuacha unafiki wa kuogopa kupoteza nafasi au vyeo.

🔊 “Sauti ya haki haifungwi. Hili si suala la dini wala itikadi – ni suala la utu na uzalendo.”

By admin

Leave a Reply