CCM: Ubaya Ubwete Na Sio Ubaya Ubwela

HIKI WANACHOKIFANYA CHAMA TAWALA NI UBAYA UBWETE NA SIO UBAYA UBWELA:

Hivi unajua ya kuwa huu msemo unafaa Sana kwenye huu uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Vijiji?unajua kuwa kinachoendelea ni ubaya ubaya na sio ule Ubaya Ubwela wa Simba sports club?

Sasa ipo hivi wakati Chama Tawala kinaleta mambo ya panya yaani kuuma na kupuliza basi Vyama mbadala(upinzani)wao wanakuja na kauli ya wee huogopi?(yanga Afrika),hii kauli inapaswa iingie masikioni mwa Chama Tawala maana kinachofanyika huwezi kukitenganisha nao.

Imefika mahali ukiwa mpinzani ni kama mtenda dhambi kwenye hii nchi Huku ukiwa Chama Tawala basi wewe ni Mtakatifu bila kuhudhuria nyumba za Ibada.

Ushauri wa Bure tu kwanini Kama upinzani hauhitajiki Bado tunang’ang’ania mfumo wa Vyama vingi? kwanini tunatumia neno Demokrasia kwenye kitu hamna? ushauri mzuri turudi tulipokua 1991 kurudi nyuma yaani Chama kibaki kimoja tu.

Kama ni kushindana, tushindane kwa ushawishi tunica tumesimama kwenye uwanja tambalale. Tushindane kwa sera, na kwa kuzingatia kuwa sote ni vyama vya siasa vyenye mapenzi mema kwa nchi yetu. Nia yetu ni kuwa na Tanzania yenye usawa, haki, usalama, na heshima kama nguzo za uimara na maisha bora. Pale tunapojisahau kuwa chama chetu ni taifa na kuwa ni Chama chetu kinachostahili heshima na tunachokiamua ndicho kinakua sheria ya nchi, basi tunajisahau kuwa na sie ni chama cha siasa kama vilivyokua vingine. Kuwa hii nchi ya Tanzania sio yetu peke yetu Bali ni ya sote na wote waliopo humu nchini, raia na si raia, wabastahili kupata heshima, usalama, na haki. Hatutoweza Kalinga na kudumisha hizi nguzo kama hatutojitambua na kujishika kama chama pale sheria inapotuongoza kuwa chama cha siasa has kipindi cha uchaguzi.

Kama uchaguzi mdogo upo hivi VIPI uchaguzi Mkuu wa kuwachagua Madiwani, Wabunge na Rais itakuaje maana hii Hali ni ya kuogofya Sana Kwa Wananchi na Vyama vyao maana watu wanakoseshwa sifa Huku sifa wanazo.

Mwisho Kabisa tujiulize kutokea 2019 mpaka Sasa Viongozi wote WA nyanja zote walitokea Chama kimoja je Wapi tulifanikiwa kama Nchi na ililipa vipi kuwa na Viongozi wa mlengo mmoja?hatuoni kama Kuna haja Sasa ya kuacha UVYAMA na tukasimama na Utaifa wetu YAANI tuwe wazalendo Kwa Nchi YETU mama Tanzania.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *