Ngara: Sakata la Pikipiki Ngumzo Mitaani

By admin May 31, 2024

SIRI ZA CCM – NGARA ZAVUJA ZOEZI LA UGAWAJI WA PIKIPIKI NYUMBANI KWA MBUNGE: MWENYEKITI NA KATIBU CCM (W) WATAJWA KUKIUZA CHAMA

Na Titho P.

Chama cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Ngara Mkoani Kagera kikiwa katika hafla ya UGAWAJI wa Pikipiki za chama kwa viongozi wa kata kwenye jengo binafsi la Mbunge kimejikuta katika sintofahamu baada ya mipango yao ya siri kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa kuvuja. Hali hii imetokana na uratibu mbovu pamoja na usimamizi wa hovyo wa zoezi hilo, usimamizi ambao haukuhusisha taratibu, miongozo wala kanuni zozote za Chama cha Mapinduzi (CCM).

Wasiwasi umetanda kwa wajumbe pamoja na wanachama wa CCM ndani wilaya ya Ngara kiasi cha kukosa uaminifu tena kwa viongozi wakuu ndani ya CCM – NGARA akiwemo Mwenyekiti wa CCM (W) na Katibu wake. Chanzo cha kutanda kwa wasiwasi huo ni kitendo cha jengo binafsi la Mwanasiasa (Mbunge) kutumika kwa shughuli za kichama kinyume na maadili pamoja na ilani ya chama chake.

M/Kiti wa CCM (W) NGARA na Katibu wa CCM (W) NGARA upendo waliouonyesha kwa Mheshimiwa Ruhoro NI MKUBWA SANA. Lakini kosa lao kubwa ni kitendo cha kuvunja ilani ya chama na kufanya Mambo ya maamuzi pasipo kushirikishana na ngazi zingine za kiutawala ndani ya chama.

SIKILIZA audio hiyo kwanza ili uendelee kusoma ukiwa na faraja!

Tukisema CCM – NGARA imemilikiwa na Mbunge (Mheshimiwa Ruhoro katika kila inachokifanya na haina mvuto kwasasa, mtasema mtu anamuonea na ana vita na yeye.

 1. IPO wapi thamani ya katibu wa CCM (W) NGARA?
 2. IPO wapi thamani ya Mwenyekiti wa CCM (W) NGARA ?
 3. UPO WAPI ushirikishwaji wa viongozi na uongozi ndani ya CHAMA ?
 4. Kuna nini nyuma yenu viongozi wakuu wa chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ngara hadi mtaani kujae sintofahamu ya juu sana kiasi hicho ?
 5. Je hivi mnajua kama wengi wa mliokuwa mkiwahubiria hapo nyumbani kwa Mbunge walikuwa wanatabasamu na kuvumilia kwa ajili ya pikipiki ?

Leo hii M/KITI na KATIBU wa CCM (W) Ngara mnaamua kushikamana kwa pamoja kuyabeba majukumu ya chama kwenye jengo la mtu binafsi (Tena mgombea wa ubunge uchaguzi ujao) huku mkijua kuwa kufanya hivyo ni kosa na ni kufifisha zitihada na michakato ya uhuru na ustawi wa kidemokrasia ndani ya Jimbo letu la Ngara.

Uongozi wa CCM mkoa wa Kagera huenda ukawa umebariki michakato hiyo na kila kinachozidi kuendelea katika taswira ya namna hii.

Mbunge wa Ngara kwa kushirikiana na Katibu wa CCM (W) NGARA pamoja na Mwenyekiti wa CCM wilaya walikuwa wameshalenga kuutumia upokeaji huo wa pikipiki kama kisemeo (platform) cha wao kujitangaza na kujinadi kama sauti inavyojithibisha yenyewe pasipo kuacha shaka lolote.

 1. Gharama za oili kila pikipiki moja lita moja.
 2. Kula na kunywa
  Pamoja na mambo mengine.

Ewe Katibu wa CCM (W) endelea kutokuwajibika pamoja na M/Kiti wa CCM (W). Kitendo chenu kama viongozi wakuu wa chama (CCM) ndani ya wilaya ya Ngara kubariki kampeni za mapema zilizoongozwa na Mathias Elias Mgata huku mkiwa mnaitambua vema miongozo yote ya chama Cha Mapinduzi mkatae msikatae, RUHORO ameshakimiliki chama, na sasa ni chake!

MTASEMA HAVINIHUSU, ILA:-

 1. Mimi ni mdau wa siasa safi na zenye kujali utii wa sheria, kanuni na taratibu zote.
 2. Mwenyekiti na KATIBU CCM (W) NGARA WOTE NI WABABAISHAJI.
 3. Kiongozi yeyote asiyeheshimu maamuzi ya wenzake ( katika ushirikishwaji wa Mambo ya pamoja) utawala wake utakuwa wa mawenge mawenge tu mwanzo mwisho AWEKWE PEMBENI!
 4. Uongozi wa CCM mkoa wa Kagera mhojini Katibu wa CCM Ngara pamoja na Mwenyekiti wake mjiridhishe kujua kama kweli maamuzi na mienendo yao yanalenga kujenga chama na siyo kumjenga mtu chini ya mwamvuli wa chama!

Uhalali au uharamu wa kisiasa katika nchi hii vitatokana na uhai wa wanasiasa wenyewe katika kusimamia na kuenzi misingi iliyowekwa na waasisi wetu.


Njaa ni ya muda mfupi ila heshima ni ya kudumu. Tujiheshimu Kisha tuwajibike ipasavyo!

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *