Katibu Mtaafu Ataka Udiwani Kibimba

By admin May 3, 2025
Ndugu Jeventus Juvenary Anatarajia Kutosa Jina Lake Kwenye Kinyang'anyiro cha Udiwani, Kata ya Kibimba

WAANDISHI WA HABARI WATANGAZA KUMCHUKULIA FOMU MWANDISHI MWENZAO JUVENTUS JUVENARY ILLAMBONA KUGOMBEA UDIWANI KATA YA KIBIMBA

Na, Bankanzako Ruguna

Ngara, Kagera – May 3, 2025

Kundi la waandishi wa habari kutoka wilayani Ngara mkoani Kagera limetangaza azma ya kumchukulia fomu ya kugombea nafasi ya Udiwani katika Kata ya Kibimba mwandishi mwenzao maarufu, Juventus Juvenary Illambona, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kuhamasisha ushiriki wa wanahabari katika uongozi wa kisiasa.

Mwandishi na mtu wa watu aamua kuweka mic na mawaya waya pembeni ili atumikie Kata ya Kibimba kama Diwani. Akiongea na gazeti hili, ametaarifa umma kuwa jina lake litakua miongoni mwa wawania udiwani Kibimba. Kutonana na muda wake kwenye tasinia ya uandishi wa habari, wandishi wa habari wameahidi kumchulia form mwandishi mwenzao ndugu Jeventus Juvenary Illambona.

Uamuzi huo umetangazwa rasmi leo katika mkutano uliofanyika mjini Ngara, ambapo waandishi hao walieleza kuwa Illambona ni kiongozi mwenye maono, anayefahamu changamoto za wananchi wa Kibimba na mwenye uwezo wa kuibua na kusimamia maendeleo ya kata hiyo.

“Tumeamua kumchukulia fomu Juventus kama ishara ya imani yetu kwake. Amefanya kazi kwa ukaribu sana na jamii, anafahamu matatizo ya wananchi na ana uwezo mkubwa wa kuwasemea,” alisema mmoja wa waandishi hao, Godwin Bruchard, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya kampeni hiyo.

Juventus Juvenary Illambona, ambaye ni mwandishi na mtangazaji wa  wa muda mrefu kwenye kituo cha Redio Kwizera, na vyombo vingine vya habari, amepokelewa kwa shangwe na wakazi wa Kibimba baada ya taarifa hiyo kusambaa. Akizungumza kwa kifupi, Illambona alieleza kushukuru kwa heshima hiyo na kusema atatoa msimamo wake rasmi hivi karibuni.

Katibu Mtaafu wa Mbunge wa Ngara, ndugu Juventus Juvenary Illambona akiwa anatumika kama nguzo muhimu ya Mheshimiwa Ndayisaba alipokua akitumika kama Katibu wake. Ndugu Juventus yupo kushoto mwenye mic na t-shirt ya rangi ya ugoro. Amepata baraka zote kutoka kwa boss wake wa zamani, kutoka kwa wananchi na wafanyakazi wote aliofanya nao kazi.

Endapo atakubali ombi hilo, Illambona atakuwa miongoni mwa wanahabari wachache waliopata sapoti ya moja kwa moja kutoka kwa wanahabari wenzao kuingia kwenye siasa za moja kwa moja, hatua inayoashiria mabadiliko ya mtazamo kuhusu nafasi ya vyombo vya habari katika maendeleo ya jamii.

Mwanahabari mwingine nguli anayeshughulika na mitandao ya kijamii Baraka Silvanus Elia amesema ni muda sasa wa Wanahabari kuingia katika majukumu ya kiserikali wakitumia taaluma zao kurekebisha,kukosoa na kuwa mfano wa Uongozi.

Ndugu Jevenary Juventus Illambona akiwa amefatwa na wazee na majirani kumpongeza kwa uamzi wa kuwania kiti cha udiwani wa Kibimba. Kama ni mtu wa watu, wana Kibimba wote wamefurahi kusikia kijana wao amekubali kuweka shughuli zake zote pembeni ili atumikie watu na jamii ya Kibimba. Ndugu Jeventus Juvenary Illambona amepatiwa neema tele kutoka kwa ndugu na jamaa.
Moja ya kazi ambazo ndugu Juventus Juvenary Illambona aliyoifanya kwa utiifu wa juu na ukamilifu ni tasinia ya Habari. Ameshafanyia kazi vituo vya radio na television, hapa na nje ya wilaya ya Ngara. Baadhi ya vyombo vya habari alivyofanyia kazi ni Radio Kwizera na Simamiatv. Hii picha ilichukuliwa studio akiwa katika ubora wake kwani ameshaweka nyenzo za utangazaji pembeni ili asikilize na kutatua kero za wana Kibimba.

Mheshimiwa mtarajiwa, Diwani wa Kibimba Juventus Juvenary Illambona akiteta na wananchi mbali mbali maswala yanayoikumba Ngara. Ushirikiano na watu mbali mbali, kuwa mtu wa watu, kutumikia kwa moyo mkunjufu hata kwa wale ambao ni hawakutani ukurasa mmoja kisiasa kwani kiongozi ni kiongozi wa wote.

By admin

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *