Hivi Sasa kumekua na vuguvugu la kisiasa katika maeneo mbalimbali ya Nchi ya Tanzania huku Kwa upande wa Jimbo la Ngara mambo yapo bambam.
Kwa sasa inafahamika Jimbo la Ngara lipo chini ya MH Mbunge Ndaisaba George Ruhoro ambae aliingia mdarakani Mwaka 2020 na atamaliza muda wake 2025.
Ikiwa umebaki mwaka kabla ya kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge, na Madiwani. Kwa Jimbo la Ngara inaonekana nafasi ya Ubunge kuhitajika na wimbi la wanasiasa mbalimbali.
Kuna viongozi waliowahi kuwa Wabunge nao bado wanautaka na hata wasiowahi kuwa wabunge nao wanautaka yaani kiufupi Jimbo la moto.
Aliyepo madarakani anawahofia waliopo nje huku waliopo nje wakijitafuta na kutafuta ushawishi chini Kwa chini.
Aliyepo madarakani anayo nafasi ya kufanya mikutano na kukutana na watu wa makundi lika mbalimbali lakini wale wanaoitwa wasaka ubunge nafasi hawana lakini bado wanayo fursa kujitambulisha kwa njia wazijuazo wao. Maana wakisema wasubirie muda ufike hayupo atakaewajua kutokana na muda kuwa finyu.
Inafahamu chama kina utaratibu wake na hakiruhusu kampeni kabla ya uchaguzi lakini haikatazi watu kujuana na watu wenzao iwe kwa kwenda misibani ama sehemu nyingine maana; bado wote ni Wanajamii ya Ngara.
Kuna hurka ya watu waliopo karibu ya Mbunge kuwaita watu wanaoenda jimboni ama Wilayani. Waliozaliwa ama wenye vinasaba na Ngara kuwa ni wasaka ubunge, jambo ambalo sio sahihi maana wanarudi kwao kutembea na kusalimia ndugu. Hata kama wanautaka ubunge bado sio dhambi na ni haki yao na hayupo mwenye hati miliki ya Jimbo la Ngara.
Mpaka sasa wanaoutaka ubunge ni wengi ila kuna orodha ya waanoutaka na Ngaratv itawaweka katika makala zijazo.
Kwa sasa kelele zimekua nyingi kwenye mitandao ya kijamii na hata mitaani huku timu mbili kubwa zikionekana kuwa zinapewa kipaumbele jambo ambalo wapo wanaoishi kwa presha kila uchwao.
Aliyepo Madarakani anahofia kuipoteza nafasi yake na aliyepo nje anaitaka nafasi hiyo jambo ambalo limeonyesha mnyukano mzito mpaka kupelekea kugawana Timu ama Makundi ya watu.
Mwisho kabisa mpaka sasa Jimbo la Ngara linaongozwa na Ndaisaba lakini kwa namna mambo yalivyo ni 50 Kwa 50 yaani arudi ama asirudi na mbichi